Katibu mkuu wa umoja wa mataifa: makubaliano ya nyuklia nilazima yahifadhiwe

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa: makubaliano ya nyuklia nilazima yahifadhiwe

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa amesema: makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran ni moja ya makubaliano makubwa ya kidiplomasia hivyo ni lazima yahifadhiwi

Shirika la habari AhlulByt (a.s) ABNA: katibu mkuu wa umoja wa mataifa “Antonio Guterres” amemtaka Rais wa Marekani “Donald Trump” kwaajili ya kuizuia Iran kumiliki silaha za Nyuklia, abaki katika makubaliano ya nyuklia na serikali ya Iran.
Aidha ameyasema hayo alipokuwa anafanya mahojiano na Televishen ya BBC na kusisitiza kuwa: laiti yasingalifikiwa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran mwaka 2015 kulikuwa na uwezekano mkubwa wakutokea mapigano.
Aidha amesisitiza kuwa: makubaliano ya mpango wa nyuklia na Iran, ni katika makubaliano muhimu ya Kidiplomasia yaliofanyika duniani ambapo ni wajibu kuyahifadhi na kuyalinda, hivyo madamu haijapatikana njia nyingine bora zaidi ya makubaliano hayo, hivyo si sahihi kuyasambaratisha makubaliano hayo, kwani tutaingia katika sehemu mbaya hatari kwa kitokea vita. Kabla ya hapo pia kiongozi huyo daima amekuwa anasisistiza kuendelezwa na kuyahifadhi makubaliano hayo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky