Kauli ya Jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) ya kukemea mauaji ya waislamu wa Myanmar

Kauli ya Jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) ya kukemea mauaji ya waislamu wa Myanmar

Jumuia ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) imetoa kauli nzito katika kukemea mauaji ya Waislamu wa Myanmar, huku ikizitaka jumuia za haki za binadamu duniani kufanya maamuzi ya haraka hata kuhakikisha kusitishwa haraka iwezekanavyo mauaji hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kufuatia kukithiri kwa mateso na mauaji ya Wailsamu wa Myanmar, jumuia ya kimataifa AhlulBayt (a.s) imutoa kauli ya kulaani na kupinga mauaji hayo nakuzitaka za haki binadamu duniani kuingilia kati na kutatua suala hilo.
Katika sehemu za ujumbe huu imeelezwa kwamba: watu wa Rohingya kwa muda mrefu wamekuwa wakidhulumiwa kwa kisingizio cha kutothibiti utaifa wao, vitendo vya ukatili dhidi yao vinafanya na mabudha wenye msimamo mkali na kuungwa mkono na majeshi ya nchi hiyo ambapo, nyumba zao, misikiti na maduka yao huchomwa moto, huku wakitolewa kwa nguvu katika makazi yao ambayo wamizaliwa na kukulia.
Ujumbe kamili wa kauli hiyo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la mwenyezi Mungu mwangamizaji wa majabbari (mabeberu)
Hatua mpya ya unyama, mauaji na mateso zimeanza dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika wilaya ya Rakhin nchini Myanmar, huku serikali ya zakimagharibi na jumuia za kutetea haki za ziliokuwa chini ya serikali hizo za kibebero zikiwa na kigugumizi katika kulielekea suala hilo.
watu wa Rohingya kwa muda mrefu wamekuwa wakidhulumiwa kwa kisingizio cha kutothibiti utaifa wao, vitendo vya ukatili dhidi yao vinafanya na mabudha wenye msimamo mkali na kuungwa mkono na majeshi ya nchi hiyo ambapo, nyumba zao, misikiti na maduka yao huchomwa moto, huku wakitolewa kwa nguvu katika makazi yao ambayo wamizaliwa na kukulia.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi hivi mwishoni zinaashiria kuwa idadi ya waliopoteza maisha katika wiki moja ya mwisho ni watu 400, katika hali ambayo mamia ya wananchi hao waliuliwa wakiwa wanakimbia au walipokuwa wanalazimishwa kuondoka walipoteza maisha kwa kuzama katika maji.
Hivyo Jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) kutokana yakwamba inawachama wengi amao ni wanazuoni na wataalamu katika mambo mbalimbali, inalazimika kuwazindua walimwengu katika mambo yafuatayo:
1.    Msngi wa dini ni kumpwekesha mwenyezi Mungu, kuwa na tabia njema, upendo na kuishi kwa amani wanadamu wote, hivyo basi kikundi chochote au serikali yeyote inayouwa wanadamu, iwe didi yeyote hile, hiyo ni dini ya uongo.
2.    Haki za awali kwa mwananchi ambazo hazina shaka ndani yake, ni maji na Ardhi ambapo katika haki hizi hakuna mtu anaetilia mashaka na i haki za asili kwa kila taifa amapo makubaliano ya kimataifa yanathibitisha haki hizo.
3.    Endapo ikatkea katika serikali yeyote kuwa wananchi fulani katika taifa lao haujathibiti utafa wao, katika hali hiyo serikali hiyo aina haki ya kuwauwa, kuwachoma moto na kuwafukuza.
4.    Hii ni katika hali ambayo, katika mataifa mbalimbali tunashuhudia zinawakaribsha wakimbizi mbalimbali kutoka mataifa tofauti, amao hukimia vita na hali mbaya ya usalama, hivyo ni jambo la kustaajabisha kwa serikali ya Mnyamar kuona linauwa wananchi wake ambao makumi ya miaka wamezaliwa na wameishi katika taifa hilo, eti kwa kuwatuhumu kuwa si wananchi halali wa nchi hiyo.
5.    Pamoja na kuwepo wafuasi wa dini ya Budha, pia hatupaswi kusahau uharbufu wa makundi ya kigaidi yaliokuwa na nemo ya Uislamu, ambavyo vinasaidiwa misaada malimbali katika ukanda wa mahariki ya kati, vikundi ambavyo vimesababisha chuki ulimwenguni dhidi ya Uislamu, amavyo havina huruma kwa Muislamu, Mkristo, Budha wala mfuasi wa dini yeyote, amapo hivi sasa pia tunashuhudia kuanzishwa fitina yengine kutoka kwa mayahudi na wazayuni katika kujenga uadui baina ya Waislamu na Mabudha ulimwenguni.
6.    Ukiangalia kwa upande mwingne serikali ya Marekani ambaye inayodai kuwa ndio kinara wa wakusimamia haki za binadmau, ambapo likitokea tatizo dogo kutoka kwa Waislamu, husimama na kutoa povu ulimwenguni likishika bendera ya kutetea haki za binadamu, hali yakuwa mpaka sasa i zaidi ya miaka mitano ya kuanza mauaji dhidi ya waislamu Mnyamar, ambapo wameamua kukaa kimya kama hawaoni yanayojiri nchini humo.
7.    Kwa upande mwingine tunaitaka jumuia ya umoja wa Waislamu na mataifa ya Kiislamu kulichukulia umuhimu suala hili, kwa kutoa shiikizo kwa serikali ya Mnyamar na jumuia za kimataifa za haki za binadamu, kusitisha mauaji yanaoedelea nchi humo dhidi ya wananchi wachache wanaoshi nchini humo, kama alivyosema kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Imam Khamenei katika ujumbe wake kwa mahujaji wa mwaka huu ambapo alisema: kupambana ipasavyo katika kuwasaidia Waislamu wachache wanaodhulumiwa, kama vile wanaodhulumiwa nchini Mnyamar, ni wadhifa wa viongozi wa nchi za kiislamu na wanazuoni pamoja na wanasiasa waliopo katika mataifa ya kiislamu.
8.    Pamoja ya kutahadharisha serikali ya mnyamar kunako tija ya mauaji haya, nashauri pande mbili zote kukaa pamoja na kutafuta njia ya kulitatua suala hilo chini ya misingi ya utu na taibia na kufuata kanuni za kimataifa.
9.    Mwisho nawaomba watu wote huru na waislamu ulimwenguni, kutoa sauti ya kupinga mauji hao, pangine tunaweza kuamsha hisia halisi ya ubinadamu kwa walimwengu, hatimaye tukaweza kuzuia kufanyika dhulma kwa mwanadamu kwa jina la dini.
لَّذينَ أُخرِجوا مِن دِيارِهِم بِغَيرِ حَقٍّ إِلّا أَن يَقولوا رَبُّنَا الله وَلَولا دَفعُ الله النّاسَ بَعضَهُم بِبَعضٍ لَهُدِّمَت صَوامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَواتٌ وَمَساجِدُ يُذكَرُ فيهَا اسمُ اللَّهِ كَثيرًا وَلَيَنصُرَنَّ الله مَن يَنصُرُهُ إِنَّ الله لَقَوِيٌّ عَزيز(surat Haji: 40)
Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.
Jumuiaya ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s)
5/9/2017
   


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky