Kauli ya jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt kuhusu kupitishwa kwa Muuswada wa kuunda “Taifa la Kiyahudi”

Kauli ya jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt kuhusu kupitishwa kwa Muuswada wa kuunda “Taifa la Kiyahudi”

Jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) pamoja na kupinga hatua hiyo ya kibaguzi na ukandamizaji, imesisitiza na kuwataka watu kuungana na Wapalestina na kukabiliana na mpango huo hata kufikia kuikomboa sehemu takatifu ya Quds

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kufuatia kupitishwa kwa muswada wa dhulma na udhalilishaji wa kuasisiwa kwa “Taifa la Kiyahudi” katika bunge la utawala haramu wa Israel, kwaajili hiyo jumuia ya kimataifa  ya AhlulBayt (a.s) imetoa kauli nzito ya kupinga hatua hiyo.
Katika kauli hiyo pamoja na kukemea hatua iliochukuliwa ambayo ni yakibaguzi na ukandamizaji, imesisitiza kuongeza ushiriakiano na wananchi wa Palestina katika kukabiliana na kutekelezwa kwa mpango huo wa kiazayuni wa kuvamia maeneo ya Wapalestina.
Kauli hiyo ni kama ifuatavy:
Kwajina la mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu
Mwenyezi Mungu anasema: kwa hakika kamwe mayahudi na wakristo hawataridhika nawe mpaka utakapo fuata mila zao, sema hakika ya uongofu wa mwenyezi Mungu ndio uongofu wa kweli, hivyo kama utafuata matakwa yao baada ya kukufikia elimu, kwa hakika mwenyezi Mungu hatakusimamia wala kukunusuru (Baqara: 120).
Hatua iliochukuliwa na Bunge la utawala haramu wa kizayuni wa kupitisha muswada wa kutengeneza “Taifala Kiyahudi” ni ishara ya kuwepo ubaguzi na chuki kwa dhidi ya Wapalestina na sehemu tukufu ya msikiti wa Quds, maana ya kupitisha mswada huo ni kwamba makazi ya wananchi wa Palestina ni miliki ya Mayahudi, jambo ambalo linakwamisha juhudi ya kuwepo taifa linaloitwa Palestina.
Kwa mujibu wa  kupitishwa kwa muswada huo hatari, utawala haramu wa Israel baada ya muda utakuwa na haki ya kuwaondosha waarabu wote wanaokaa Palestina, kuwafukuza nchini humo hususan wale wanaoishi sehemu ya Quds mashariki na ukanda wa Gaza, jambo ambalo litapelekea kukosa makazi mamilioni ya Wapalestina...nk
Hivyo basi jumia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) baada ya kulaani hatua hiyo, inatoa wito wa kuendelea kukabiliana na hatua hiyo na kushirikiana na Wapalestina na wale wote wanaopenda uhuru na kuikomboa Quds tukufu, na kuyepuka mazungumzo yeyete ya kuweka mafungamano na utawala haramu wa Israel.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky