Kikundi ch kigaidi cha Daesh chawachinja wataleban kumi nchini Afghanistan

Kikundi ch kigaidi cha Daesh chawachinja wataleban kumi nchini Afghanistan

Magaidi wanaofungamana na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika wilaya Juzjani nchini Afghanistan wamewachinja watu kumi wa kikundi cha kigaidi cha Taleban ikwemo mmoja kati yao ni katika makomanda wa kikundi hicho

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: watu kadhaa wanaofungamana na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika wilaya ya Juzjani wameuwa kwa kuwachinja watu kutoka kikundi cha kigaidi cha Taleban nchini humo.
Viongozi wa wilaya hiyo baada ya kuthibitisha habari hiyo amesema kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji cha Aq-Bilaq kiliopo katika mkoa wa Darzab nchini Afghanistan.
“Bazi Muhammad Davar” kamanda mkuu wa mkoa wa Darzab katika wilaya ya Juzjan ameviambia vyombo vya habari kuwa: magaidi wa kikundi cha Daesh waliwakamata watu 10 kutoka katika kikundi cha kigaidi cha Taleban ikiwemo miongoni mwao kamanda mmoja siku nne ziliopita na baada ya siku kadhaa ndio waliamua kuwauwa kwa kuwachinja.
Mkoa wa Darzab nchini Afghanistan ni katika mikoa isiokuwa na amani nchini humo katika wilaya ya Juzjan, ambapo hapo kabla viongozi wa wilaya ya Juzjan imevamiwa na magaidi wa kikundi cha Daesh, ambapo viongozi hao waliitaka serikali kuu kujaribu kujipanga vizuri katika sehemu hiyo katika kukabiliana na kikundi hicho cha kigaidi nchini Afghanistan.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky