Kikundi cha Daesh chathibitisha kuangamia kwa kiongozi wao mkuu (Albaghdadiy)

Kikundi cha Daesh  chathibitisha kuangamia kwa kiongozi wao mkuu (Albaghdadiy)

Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimetoa kauli fupi inayosthibitisha kuangamia kwa kiongozi mkuu wa kikundi hicho ch kigaidi Abubakari Albaghdadiy, huku wakisisitiza kuwa baada ya muda mchache atatangazwa kiongozi mwingine

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimeatoa ripoti ambayo inathibitisha kuangamia kwa Abubakari Albaghdadiy ambaye ni kiongozi mkuu wa kikundi hicho na kusisitiza muda si mrefu atatangazwa kiongozi mpya wa kikundi hicho.
Shirika la habari la Alsumariyah nchini Iraq siku ya Jumanne likinukuu kutoka kwa chanzo kimoja kiliopo katika mkoa wa Nineveh ametangaza kuwa: katika kauli mpya ya kikundi cha kigaidi cha imetangazwa rasmi kuangamia kwa kiongozi wa kikundi hicho Abubakari Albaghdadiy.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimewataka watu wake wabaki katika makambi na maeneo ambayo yako chini yao na kuepuka hali ya kutoka katika maeneo hayo.
Aidha kikundi hicho siku mbili ziliopita kilitanga kuzuia kutangaza kuangamia kwa kiongozi huyo, ambapo tangazo hilo lilitolewa katika mji wa Tachl Afar nchini Iraq na kusisitiza kuwa yeyote atakaye zungumzia kifo  kiongoi huyo, hukumu yake ni viboko.
Taarifa hii imesambaa katika hali ambayo kwa kawaida kikundi cha kigaidi cha Daesh mara nyingi hutangaza habari ziliokuwa na uhakika kwao, katika shirika la habari la Aamaq kitu ambacho hawajatumia katika kutangaza habari hii.
Kwa upande mwingine shirika la kinataifa la haki za binadamu limethibitisha kuangamia kwa kiongozi wa kikundi hicho nchini Syria, ambapo leo wametoa tangazo lakuthibitisha kuangamia kwa Abubakari Albaghdadiy, huku wakashiria kuwa wadalili nzito zinazothibitisha hilo.
Wizara ya ulinzi ya Urusi muda mrefu ilikuwa imeshatangaza kuangamia kwa kiongozi kufuatia shambulio la anga liliofanywa na majeshi ya nchi hiyo katika sehemu ambayo hujumuika makamanda wakuu wa kikundi hicho cha kigaidi sehemu ya Hume ya Raqqa nchini Syria, ambapo baada ya hapo Marekani ilipinga vikauli hiyo na kusema kuwa si sahihi kuwa kiongozi wa kikundki cha kigaidi cha Daesh kuangamia kwa shambulio hilo, ama baadhi ya nchi za Ulaya zilionekana kuwa na mashaka katika suala la kuangamia kwake.
mwizho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky