Kikundi cha Daesh wauwa wairaq kadhaa kwa kuwachoma moto

Kikundi cha Daesh wauwa wairaq kadhaa kwa kuwachoma moto

Kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq chafanya tukio la kusitisha nchini humo ambapo limewakamata wananchi wa kawaida wa kaskazini mwa Iraq na kuwauwa kwa kuwachoma haliyakuwa wako hai

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habari la Sumariay limetangaza katika ripoti zake likinukuu kutoka kwa vyanzo makani vya usalama katika mkoa wa Karkuk kaskazini mwa Iraq amesema kuwa: wananchi 12 wameuliwa kinyama na kikundi cha kigaidi cha Daesh kwa kosa la kutoroka katika mji wa Huwejeh uliopo kusini mwa magharibi mwa mkoa huo nchini humo.
Aidha chanzo hicho kimetangaza kuwa: wanamgambo wa Daesh walikamata wananchi 12 usiku wa Jumamosi ikiwemo miongoni mwao watu wanne kutoka familia moja waliwachoma moto kwa kosa lakukimbia sehemu ya mji wa Huwejeh.
Aidha chanzo hicho kisiotaka jina lake litajwe amesema: watu hao walitekwa walipokuwa wanakimbia kwenda mji unaottwa Al-elmu uliopo mashariki mwa mkoa wa” Saladin” ambapo baadae wakawaingiza katika matundu ya chuma na kuwamwagia mafuta hatimaye kuwachoma moto.
Mji wa Hawijah, Rashad, Al-zab, Alriyadh na Alabasiy iliopo kusini mwa magharibi mwa Kirkuk zilitekwa na magaidi wa Daesh mnamo mwezi juni mwaka 2014 na mpaka sasa wakazi laki moja na hamsini wametoroka sehemu hizo, kitu ambacho kina wakasirisha magaidi wa kikundi cha hicho cha Daesh hatimaye kufanya vitendo vya kinyama kama hivyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky