Kikundi cha Hamasi na Fathi wafanya suluhu na kusaini rasmi makubaliano

Kikundi cha Hamasi na Fathi wafanya suluhu na kusaini rasmi makubaliano

Kikundi cha Hamasi na Fathi wafanya suluhu nchini Misri na kusaini mkataba rasmi baina ya vikundi hivyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: adhuhuri ya leo Alhamisi kumefikiwa makubaliano na suluhu baina ya Hamasi na Fathi baada ya mazungumzo mapana yaliofanyika kwa muda wa siku 3, hatimae kufikia muafaka wa ktaifa, kikao na mazungumzo hayo yalifanyika Cairo, mji mkuu wa Misri.
Muafaka huo umefanywa katika mako makuu ya shirika la usalama la Misri, likiwa kama msimamizi mkuu wa makubaliano hayo, ambapo ilifanya juhudi kubwa za kuyakusanya makubndi hayo mawili ya Palestina mpaka kufikia kusaini makubaliano ya pande hizo nchini Misri.
Hii ni katika hali ambayo Ismail Hania kiongozi wa kikundi cha Hamasi, asubuhi ya leo alitoa habari yakufikia makubaliano ya hayo kati ya Hamasi na Fatih, ikiwa ni tija ya mazungumzo yaliofanyika mjini Cairo kuanzia siku ya Jumanne chini ya serikali ya Misri.
Aidha Hania katika mazungumzo yake mafupi alisema vikundi viwili (Hamasi na Fathi) vimefikia makubaliano chini ya usimamizi wa nchi rafiki ya Misri.
Fathi na Hamasi hapo kabla vilitoa tamko kuwa kuna mazingira mazuri ya kufanya mazuri yakuweza kufikia makubaliano ya pande hizo mbili hatimae kufikia muafaka wa kitaifa, huku wakisisitiza kuwa tunamuomba Mungu aifanye hali hiyo iwe yenye kuendelea hata kufikia makubaliano ya mwisho.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky