Kikundi cha kigaidi cha Boko Haramu chamuua mkuu wa shule ya msingi nchini Niger

Kikundi cha kigaidi cha Boko Haramu chamuua mkuu wa shule ya msingi nchini Niger

Wizara ya elimu na mafunzo nchini Niger imetangaza kuupata mwili wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi “Bilali Amadu” aliokuwa amechinjwa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haramu nchini Nigeria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Wizara ya elimu na mafunzo nchini Niger imetangaza kuupata mwili wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi “Bilali Amadu” aliokuwa amechinjwa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haramu nchini Nigeria.
Magaidi wa kikundi cha kigaid cha Boko Haramu walimuuwa mwalimu huyo katika kijiji cha Jaskiru kiliopo sehemu Difa kusini mwa mashariki ya Niger karibu na mpaka wa Nigeria.
Waziri wa elimu na mafunzo wa Niger ameandika katika ukurasa wake wa Facebook ameandika na kupinga vikali mauaji ya mwalimu mkuu huyo nchini humo.
Inasemekana kwamba kikundi cha kigaidi cha Boko Haramu katika mji wa Difa na maeneo mengine, walizitaka shule na walimu wa sehemu hizo kuancha kutoa mafunzo kwa watoto wa sehemu hiyo kwakile walichodai kuwa ni haramu kutoa mafunzo hayo kwa watoto.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky