Kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah azimia

Kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah azimia

Wizara ya ulinzi na usalama ya Urusi imetangaza kuwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah nchini Syria amezimia kufuatia shambulio la anga la ndege za kivita za Urusi, ambapo awali alipatwa na majaraha makubwa na hivi sasa amezimia.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi na usalama ya Urusi imetangaza kuwa “Abu Muhammad al-Jaulaniy” kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah nchini Syria amejeruhiwa na mashambulio ya anga yaliofanwa na majeshi ya Syria ambapo baada ya muda kadhaa wa kujeruhiwa kwake alipoteza fahamu na kuzimia.
Aidha wizara hiyo imebainisha kuwa, suala hilii limepelekea kutokea hali ya sintofahamu baina ya magaidi wa kikundi hicho katika mji mzima wa Adlib.
Wizara ya ulinzi na usalama ya Urusi imetangaza kuwa mashambulio makali ya wizara yalifanywa kwa muda wa masaa 24 yaliokuwa na lengo la kuangamiza magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Janhatun Nusrah ambapo mnamo tarehe 18 mwezi tisa mwaka huu walishambulia kambi ya kijeshi ya Urusi iliopo karibu na mkoa wa Adlib nchini Syria, huku Urusi akisisitiza kuwa mashambulio hayo ni yenye kuendelea.
Aidha wizara hiyo imetangaza kuwa kufuatia shambulio waliolifanya dhidi ya magaidi hao limepelekea kuangamaia kwa magaidi 49 miongoni mwao magaidi 7 ni makamanda wa kikundi hicho nchini Syria.
Kwa upande mwingine majeshi ya anga ya Urusi yamefanikiwa kugundua ghala kubwa la silaha za kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusra katika mkoa wa Adlib nchini Syria hatimaye kufanikiwa kulisambaratisha.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky