Kombora lolote la Marekani likielekezwa nchini Syria tutalisambaratisha angani

Kombora lolote la Marekani likielekezwa nchini Syria tutalisambaratisha angani

Naibu wa mkuu wa masuala ya ulinzi na Usalama nchini Urusi ametangaza kuwa, kama wanajeshi wa nchi hiyo watalengwa kushambuliwa na majeshi ya Marekani, majeshi ya Urusi itajibu mashambulizi hayo papo kwa hapo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: balozi wa Urusi nchini Lebanoni ametoa angalizo kuwa, kombora lolote la Marekani liliorushwa kwaajili ya kushambulia Syria, tutalisambaratisha kombora hilo hewani kabla ya kufika palipolengwa.
Katika habari nyingine Syria imetangaza kuwa, majeshi ya Urusi yaliopo nchini Syria, kama yatashambuliwa na shambulio lolote, bila ya kupoteza muda majeshi ya Urusi yatajibu mashambulizi hayo.
Kadhalika naibu wa mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama nchini Urusi leo ametangaza kuwa kama majeshi ya Urusi yaliopo nchini Syria yatasahmbuliwa na makombora ya Marekani, bila shaka majeshi ya Urusi yatajibu vikali mashambulio yaliofanywa.
Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa: wizara ya ulinzi na usalama imeimarisha ulinzi na uslama katika kambi za majeshi ya nchi hiyo iliopo sehemu ya Hamimi na Tartus nchini Syria, zimewekewa ulinzi wa kutosha, kwa maana hata kama watashambuliwa hawatakuwa wenye kuathiriwa  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky