Bin Salmani apigwa risasi 2 katika mashambulio yaliotokea Riyadh

Bin Salmani apigwa risasi 2 katika mashambulio yaliotokea Riyadh

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Husein Shariatimadari ameandika katika gazeti la Kayhan kuwa, kuna ushuhuda mwingi unaonyesha kuwa siku 30 za kutoonekana kwa Muhammad bin Salman si suala la kawaida, ambapo inaashiria kuwa amepatwa na tukio huku juhudi zikifanyika za kuficha tukio hilo.

 Miongoni mwa sababu na dalili hizo ni kwamba, mnamo mwezi wa nne tarehe 21 mwaka huu kulitangazwa kutokea kwa mapigano ya kurushiana risasi katika kasri ya kifalme mjini Riyadh, ama baada ya mrefu wa kusikika kwa milio ya silaha nzitu, yakaonekana majeshi ya usalama ya Saudi Arabia yamejipanga tayari kimapambano wakiwa na vifaru na vingine vya kivita, lakini baada ya muda yakakoma mapogano yale, bila ya kutangaza kuwa jambo limetokea, ama ilipofika asubuhi viongozi wa Saudi Arabia wakatangaza kwamba kulikuwa na (Ipahbad) inayotumika kwa michezo ya watoto, ilionekana juu ya Kasri hiyo ndipo wakaishambulia hata kuisambaratisha, maelezo ambayo yalipelekea watu kuingiwa na mashaka kwani haiwezekani kwa majeshi kujipanga kwa vifaru kwaajili ya kuonekana kwa kifaa cha kuchezea watoto.
Aidha baada ya hapo Muhammad bin Hakuwa mwenye kuonekana katika vyomba vya habari mpaka sasa jambo ambalo si kawaida yake, kadhalika safari ya Ghafla ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani kwenda mji Riyadh kwa madai ya kuonana na Muhammad bin Salman bila ya kuonekana hata picha moja ya mazungumzo yake na muhusika, ni katika mambo yanayoashiria jambo fulani si kawaida yake kutoonekana katika vyombo vya habari nk, huku habari za ndani zikiashiria kuwa Muhammad bin Salman kwa uchache alipigwa risasi mbili katika mashambulizi yaliotokea tarehe 21 ya mwezi wa nne mwaka huu hata kuna uwezekano mkubwa kuwa amefariki katika tukio hilo.
mwisho/290

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky