Kundi la kigaidi la Daesh lasambaratishwa nchini Iraq na Syria

Kundi la kigaidi la Daesh lasambaratishwa nchini Iraq na Syria

General Qasem soleiman wa Iran ambaye ndie muongazi mkuu wa vita hivyo dhidi ya magiadi hao nchini Syria na Iraq, aliahidi kuwaangamiza magaidi hao katika kipingi kisichopungua miezi miwili.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kundi la kigaidi la Daesh linalojiita dola la kiislamu IS linaonekana kuishiwa nguvu wakati huu ambapo makabiliano makali yanaendelea kati yao na vikosi vya jeshi na wapiganaji nchini  Iraq na Syria ambayo vinaongozwa na wataalamu wa masuala ya kijeshi kutoka Iran.

Haya yanajiri baada ya miji mikuu iliyokuwa chini ya kundi hilo la kigaidi linalodhaminiwa na Saudia arabia katika mataifa hayo kukombolewa. Sasa kuna matumaini ya ushindi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria.

Kundi hilo lililohusika na maovu chungu mzima dhidi ya raia, sasa linaonekana kusambaratishwa.

Baada ya kuwatendea ukatili wenyeji walioishi chini ya amri yao kwa zaidi ya miaka mitatu, wapiganaji hao sasa wanangángána kubakia katika maeneo madogo nchini Iraq na Syria, iliyozingirwa na wanajeshi wa ndani kutoka pande zote.

Kwasasa magaidi hao wamebaki wachache, hata hivyo, watu weengi wanatarajia kundi hilo kuangamizwa kabisa  na  umwagikaji damu kumalizika katika nchi hizo mbili na ukanda mzima.

Wacha tutazame kwa undani kikundi hicho cha dola la kiislamu, kupanda na kuathirika kwa nguvu zake za kujenga dola la kiislamu na nini cha kutarajiwa.

kundi la kigaidi la Daesh lililotokana na baadhi ya wale waliokuwa katika kundi la kigaidi la al Qaeda nchini Iraq kilianza kuenea mashariki mwa kati mapema mwaka wa 2014, kwa kuuteka mji wa Falujah na maeneo yenye kuuzunguka mji wa Ramadi.

Mnamo mwezi juni, kundi hilo likauteka Mosul ambao ni mji wa pili mkubwa Iraq, ambapo kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi alipojitangazia dola la kiislamu.

Kundi hilo likaahidi haki na usawa pamoja na kufuata muongozo wa kiislamu lakini hakutimiza hilo. Kwa miaka michache waliwatesa watu waliokuwa chini yao ikiwa ni pamoja na kuwaua na kuwanyanyasa kingono wanawake na wasichana na miongoni mwa ukatili mwengine walioufanya.

Kikundi hicho pia kilivutia watu wa kila aina wakiwemo wapiganaji wa kigeni na kuundwa kwa kundi la kigaidi la Daesh kulikuwa kwa mkakati na hatimaye ikajitanua kimataifa.

Kilichosalia

Marekani ilizindua kampeni ya mashambuzi ya angani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq mwezi Agosti mwaka wa 2014. Na mwezi mmoja baadaye nchini Syria lakini kampeni za Marekani hazikufanya lolote.

Nchini Iraq marekani ilishirikiana na vikosi vya serikali vikifanya kazi na kundi la washia pamoja na wapiganaji wa kikurdi maarufu kamapeshmerga lakini majeshi ya Marekani yalituhumwa kutoa siri na mipango ya kijeshi kwa magaidi wa Daesh. Nchini Syria Marekani ilishirikiana na wapiganaji wakisyria wanaongozwa na wakurdi SDF ambao waliungana na makundi ya kigaidi kupambana na serikali  ya Syria.

Ushindi huu mkubwa dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh na makundi mengine ya kigaidi unatokana na juhudi kubwa zilizofanywa na majeshi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran, ambayo ndo majeshi ya kwanza kuitikia wito wa kutoa msaada nchini Syria na Iraq .

Vikosi hivi vimefanikiwa kuwaondoa kundi la kigaidi la Daesh kutoka ngome moja hadi nyengine kwa miaka mingi. Pigo kubwa lilikuja mwezi Julai  wakati mji wa Mosul ambao kwa muda mrefu umeonekana kuwa mji wa utawala wa kundi la kigaidi la Daesh kuachiliwa huru.

Nchini Syria kundi la kigaidi la Daesh limeonekana kuishiwa nguvu wakati ambapo vikosi vya wapiganaji wa hizbollah wanaongozwa na majeshi ya Iran vikishirikiana na Urusi na vikosi vya serikali ya Syria vinawashambulia kwa mapigo tofauti kwa wakati mmoja.

Gharama Kubwa

Mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh umekuja kwa gharama kubwa kwa mataifa ya Syria na Iraq, na mateso makubwa kwa wale waliovumilia utawala wa kikatili wa wanamgambo hao. Mapigano na makombora ya angani yameharibu miji iliyokuwa imekuwa na kuyageuza kuwa maeneo yasiotizamika.

Wiki mbili zilizopita majeshi yanayoongozwa na Iran ya umeirudisha asilimia 94 ya ardhi iliyokuwa ikitumiwa na v kwa wananchi wa eneo hilo tangu mwaka wa 2014, na kuwaokoa zaidi ya wasyria na wairaqi milioni 6 katika mchakato huo. 

 Takriban wananchi 735 wameuawa bila kuusudia kutokana na mashambulizi ya ndege ya jeshi la muungano likiongozwa na marekani ingawa wanaharakati na wachunguzi wa vita wanakadiria kuwa idadi hiyo imeongezeka.

Katika miaka mitatu, tangu kundi la kigaidi la Daesh lianze kuunda dola la kiislamu , limewaua maelfu ya watu, limesababisha mamilioni kukimbia makazi yao na kufanya bidii kuwashawishi watoto kwa kuwafunza itikadi kali ya kidini.

Kupanuka kwa kundi hilo, na vita vya mara kwa mara pamoja na miungano iliyoundwa kuikabili kundi la kigaidi la Daesh imeathiri mweleko wa kisiasa na wa madhehebu nchini Syria na Iraq na kwa asilimia kubwa imeleta mshikamano kwa wananchi wanchi hizo .

Vikosi vyote vinavyokabiliana na kundi hilo vitalazimika kuwa macho hata baada ya kuukomboa mji wa mwisho uliyokuwa chini ya kundi la kigaidi la Daesh. Kwa namna fulani sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa zaidi. Wachambuzi wanasema wapiganaji hao watasubiri muda mwafaka kujizindua upya au kutekeleza mashambulizi ya kujitolea muhanga.

General Qasem soleiman wa Iran ambaye ndie muongazi mkuu wa vita hivyo dhidi ya magiadi hao nchini Syria na Iraq, aliahidi kuwaangamiza magaidi hao katika kipingi kisichopungua miezi miwili.

Mwisho wa habari /291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky