Maandamano yakupinga ukosefu wa ajira yaitishwa nchini Saudi Arabia

Maandamano yakupinga ukosefu wa ajira yaitishwa nchini Saudi Arabia

Wito wa kushiriki maandamano ya kupinga ukosefu wa kazi wananchi wa Saudi Arabia, yatakao fanyika siku ya Jumapili katika kila miji ya nchi hiyo

Shirika la habari AhluBayt (a.s) ABNA: wito huo umepokelewa vizuri na wanachi wengi nchini humo katika mitandao ya kijamii, wakisisitiza kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupinga ukosekanaji wa kazi kwa wananchi wa nchi hiyo.
Wito wa maandamano hayo unaanuani ya (mkusanyiko wa wasiokuwa na kazi) ambao umesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, huku wakiwataka waandamanaji kukusanyika siku ya Jumapili mkabala na ofisi yeyote inayohusika na kazi kwa wananchi.
Masiku kadhaa yaliopita kulitangazwa taarifa kama hizi katika mitandao ya kijamii nchini Saudi Arabia, ambapo pia ilipokelewa vizuri na wananchi wa nchi hiyo, ama serikali ya nchi hiyo, ilitumia mbinu ya kurejesha baadhi ya misaada iliokuwa imesitishwa kwa muda mrefu kwa wafanyakazi na majeshi ya nchi hiyo, kwa lengo la kutuliza hali hiyo.
Serikali ya Riyadh ililazimika kukata baadhi ya misaada kwa wananchi, kufuatia kupungua kwa maozo ya mafuta ya nchi hiyo kwa upande mmoja na kutoa hazina kubwa ya uchumi wa nchi hiyo kwaaji ya kuendesha vita ya Yemen kwa upande mwingine, kitu ambacho kimesababisha wananchi kukasirishwa na hali hiyo.
Serikali ya Saudi Arabia kwaajili ya kununua vifaa vya vita imetumia dola bilioni kadhaa ikiwa pamoja na washirika wake wa nchi za kimagharibi kwaaji ya kuendeleza mashambulio ya kivazi nchini Yemen, ambapo mpaka hivi sasa zaidi ya watu elfu 12 wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi hayo.
Aidha serikali ya Saudi Arabia imetoa tangazo la kuzuia maandamano hayo, huku ikiimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali katika nchi hiyo, hususan katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh.
Kwa mujibu wa ripoti ya baadhi yaviongozi wa Saudi Arabia ni kwamba vita ya Yemen imeathiri kiasi kikubwa uchumi wa nchi hiyo, ambapo kwa serikali hiyo hivi sasa imechukua hatua za kubana matumizi kwaajili ya kuziba mapengo ya uchumi yaliopo hivi sasa, kwa upande mwengine waweze kuendeleza vita ya Yemen.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky