Maelfu waandamana Barcelona kupinga kukamatwa viongozi wa Catalonia

Maelfu waandamana Barcelona kupinga kukamatwa viongozi wa Catalonia

Polisi huko Barcelona wanasema zaidi ya watu 300,000 wameandamana katika huo mji mkuu wa Catalonia kutaka kuachiwa na kurejeshwa nyumbani wanasiasa tisa waliohusika katika lile jaribio ambalo halikufanikiwa la kutaka kujitenga na Uhispania mwaka jana.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Polisi huko Barcelona wanasema zaidi ya watu 300,000 wameandamana katika huo mji mkuu wa Catalonia kutaka kuachiwa na kurejeshwa nyumbani wanasiasa tisa waliohusika katika lile jaribio ambalo halikufanikiwa la kutaka kujitenga na Uhispania mwaka jana. Waandalizi wa maandamano hayo wamesema idadi ya watu waliojitokeza ilikuwa kubwa mno kuliko makadirio yao. Maandamano hayo yanakuja miezi sita baada ya wanaharakati wa kupigania uhuru wa Barcelona Jordi Cuixart na Jordi Sanchez kufungwa jela. Watu hao wawili wanakabiliwa na mashtaka ya uasi yanayoweza kupelekea kifungo cha miaka 30 gerezani. Rais wa bunge la Catalonia na mwenzake wa chama cha utamaduni wa Catalonia kinachoshinikiza uhuru wa Catalonia ni miongoni mwa hao wanaosubiri kufunguliwa mashtaka. Makundi haya mawili ndiyo yaliyoandaa maandamano ya jana chini ya kauli mbiu "nafasi ya demokrasia na kuishi vyema." Waliungwa mkono na makundi kadhaa ingawa si makundi yote yanayopigia debe kujitenga kwa Catalonia ila yanapinga kuzuiwa kwa viongozi hao na wanataka mazungumzo baina ya Catalonia na serikali kuu iliyoko mjini Madrid yafanyike ili kuukwamua mkwamo ulioko.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky