Magaid 14 waangmia katika shambulio la majeshi ya Misri nchini humo

Magaid 14  waangmia katika shambulio la majeshi ya Misri nchini humo

Magaidi 14 waangamia kufuatia shambulio liliofnywa na majeshi ya ulinzi ya Misri katika kambi yao ya mafunzo nchini humo

Shirika la habariAhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa idai kadhaa ya magaidi hao zimetangazwa nchini Misri.
Wizara ya mambo ya ndani ya Misri siku ya Jumamosi ya tarehe 8 mwezi huu, imetoa kauli na kutangaza kuwa: majeshi ya usalama ya nchi hiyo yaligundua sehemu ambayo magaidi hao walikuwa wakipata mafunzo ya kijeshi, sehemu ambayo ipo katika mapori ya mkoa wa Ismailiyah mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Cairo, ndipo wakafanya shambulio hilo na kufanikiwa kuangamiza magaidi hao 14.
Kituo hicho kilikuwa kinatumika kutoa mafunzo ya ushupavu wa mwili, kutumia silaha na kutengeza mabomu kwa vjina wa nchi hiyo na baada ya kumaliza wajumuika na vikundi vya kigaidi na kufanya matukio ya kigaidi nchini humo.
Katika shambulio hilo majeshi ya usalama ya Misri walivamia sehemu hiyo ya mafunzo ya kigaidi na kuuwa magaidi wasiopungua 14 ambapo majina ya watano kati yao tayari yameshafahamika.
Vikundi vya kigaidi vya Daesh siku ya Ijumaa walivamia kituo cha ukaguzi cha majeshi ya Misri karibu na sehemu ya Rafah na kuuwa wanajeshi 23, huku habari zinaeleza kuwa katika shambulio hilo pia magaidi 40 waliangamia.
Tawi la kikundi cha kigaidi cha nchini Misri katika hivi karibuni, kimefanya mamia ya mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali nchini humo dhidi ya majeshi ya Misri na wananchi wake.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky