Magaid wa Daesh waangamizwa na wengine kutekwa nchini Iraq

Magaid wa Daesh waangamizwa na wengine kutekwa nchini Iraq

Wapiganaji wa kikosi cha Nujabaa ambalo ni miongoni mwa majeshi ya Iraq katika shambulio lake katika mkoa wa Saladin, wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi wa kikundi cha Daesh mkoani humo huku wengine kadhaa kufanikiwa kuwateka

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:wapiganaji wa kikundi cha Nujabaa katika majeshi ya Iraq, katika mashambulizi yao yliofanywa katika mkoa wa Saladin, pamoja na kuwaangamiza Magaidi wa kikundi hicho, wamewateka idadi kadhaa ya magaidi katika mkoa huo.
Aidha kikosi hicho cha Nujabaa baada ya kumaliza mashambulizi yao ya kuikomboa Hawija walitega mitego kaskazini mwa mkoa wa Saladin nakufanikiwa kutoa kichapo cha maana dhidi ya magaidi wa Daesh.
Kwa upande mwengine wamesema kuwa mashambulio hayo yalifanywa katika sehemu ya (Jibali Makhul) katika mkoa huo, sehemu hiyo pia kulikuwa na mahandaki ambayo magaidi wa Daesh walijificha ndani yake ambapo walisambaratisha wakiwa ndani ya mahandaki hao.
Alkadhalika wamefanikiwa kuiteka makao makuu ya kikundi hicho katika mkoa wa Saladin ambapo gaidi mmoja wa Daesh alikuwa katika juhudi za kutaka kujiripua baina ya wapiganaji wa Iraq lakini kwa uwezo wa mwenyezi Mungu hawakufanikiwa kitu ambacho kilipekea kufanikiwa kuiteka sehemu hiyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky