Magaidi 12 wa Daesh waangamizwa katika mji wa Tal Afar nchini Iraq

Magaidi 12 wa Daesh waangamizwa katika mji wa Tal Afar nchini Iraq

Majeshi ya anga ya Iraq yamefanya mashambulizi katika mji wa Tal Afar na kufanikiwa kuangamiza magaidi 12 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, miongoni mwa walioangamia ni msimamizi wa mahakama ya kikundi hicho katika mji wa Tal Afar

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia magaidi 12 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh zatangazwa nchini Iraq.
Ndege za kijeshi la Iraq zimefanya mashambulizi katika kambi moja ya vikundi vy kigaidi vya Daesh katika mji wa Tal Afar uliopo katika mkoa wa Nenaveh kaskazini mwa Iraq.
Katika shambulio hilo magaii 12 wa kikundi cha Daesh wameangamia ikiwemo kiongozi wa mahakama ya kikundi hicho katika mji wa Tal Afar.
Aidha shambulio hilo limefanywa sambamba na kutangazwa rasmi kwa kukombolewa kikamilifu sehemu ya zamani ya mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Mji wa Tal Afar ni katika miji michache ya Iraq iliopo na vikundi vya kigaidi vya Daesh, ambapo mji huo upo karibu na mji wa Musol, na magaidi wa Daesh waliingia katika mji huo toka miaka mitatu iliopita.
Baada ya kutekwa kwa mji wa Tal Afar na kikundi cha kigaidi cha Daesh, wafuasi wengi wa madhehebu ya Shia walikimbia mji huo na kuwa wakimbizi katika sehemu mbalimbali ya nchi hiyo, ambapo asilimia kubwa walikimbilia miji ya kusini mwa Iraq ikiwemo mji wa Najaf na Karbala nchini humo.
Mpaka sasa kuna maeneo machache nchraq ambayo yanakaliwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh ambapo ni maeneo ya miji ya Tal Afar.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky