Magaidi 271 wasadikiwa kurudi nchini Ufaransa wakitoka Iraq na Syria

Magaidi 271 wasadikiwa kurudi nchini Ufaransa wakitoka Iraq na Syria

Magaid wa Daesh 271 kutoka sehemu mbalimbali nchini Iraq na Syria wasadikiwa kurudi nchini kwao Ufaransa huku majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo kuimarisha ulinzi vizuri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa amesema kuwa: magaidi 271 kutoka sehemu mbalimbali za taifa la Iraq na Syria ambazo zilikuwa na machafuko, wamerudi nchini Ufaransa, ambapo vyombo vya usalama wa nchi hiyo imejipanga ipasavyo katika kubiliana nao.

Aidha waziri huyo ameongeza kusema kuwa miongoni mwa magaidi 271 waliorudi nchini humo, 217 ni watu wakubwa na 54 wana umri kati ya ujana na utoto huku wengine miongoni mwao wako katika mahabusu za nchi hiyo.

Naye alisema alipokuwa anajibu suali hili kuwa: ni wananchi wangapi wa Ufaransa waliokuwa wamejiunga na kikundi cha vikundi vya kigaidi nchini Iraq na Syria na kupoteza maisha wakiwa katika mataifa hayo? Alisema ni vigumu kutoa takwimu sahihi katika suala hilo.

Kwa mujibu wa uhakiki uliofanywa, unaonyesha kuwa watu karibu 700 kutoka nchini Ufaransa wako nchini Iraq na Syria wakifanya vitendo vya kigaidi nchini humo, ambapo serikali ya Ufaransa inachangamoto kubwa ya kutafuta njia muhimu ya kukabiliana nao watakaporudi nchini humo.

Inasemekana ni kwamba kurejea kawa magaidi wa Ufaransa walikuwa wameshiriki mauaji ya kigaidi nchini Iraq na Syria, ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa hilo pamoja na mataifa yote yaliopo bara la Ulaya.

mwisho/190


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky