Magaidi 30 wa Daesh wajiunga na kikundi cha kigaidi cha Taliban nchini Afghanistan+ picha

Magaidi 30 wa Daesh wajiunga na kikundi cha kigaidi cha Taliban nchini Afghanistan+ picha

Kundi la magaidi 30 miongoni mwa magaidi wa Daesh wameamua kuachana na kikundi hicho na kuungana na kikundi cha kigaidi cha Taliban katika mkoa wa Shirin Tegab nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: viongozi wa mkoa wa Faryab kaskazini mwa Afghanistan wametoa taarifa ya kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kimejiunga na kikundi cha kigaidi cha Taleban katika mkoa huo.
Hayo yamesemwa na (Abdulkarim Surush) msemaji wa kamanda wa jeshi la Polisi katika mkoa wa Faryab kuwa: Mufti Neematullah, mmoja katika viongozi wakubwa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, amekusanya wafuasi wake 30 na kuelekea katika mkoa wa Sirin Tegab kwaajili ya kuuungana na kikundi cha kigaidi cha Taleban.
Aidha amesema viongozi kadhaa wa kikundi cha kigaidi cha Taleban wamepinga kuwapokea magaidi hao 30 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, kadhalika Surushi ameendelea kuashiria ugomvi uliopo kati ya kikundi cha kigaidi cha Daesh na Taleban kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mapambano baina ya kikundi cha Daesh na Taleban katika mkoa huo.
Hii ni katika hali ambayo hapo mwanzo kikundi cha kigaidi cha Daesh na Taleban walishambuliana vikali katika mkoa wa Nangarhar, Faryab, Jowzjan, Zabol na baadhi ya maeneo ya Afghanistan.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky