Magaidi 5600 wa Daesh kutoka ktikia nchi 33 duniani warejea katika mataifa yao

Magaidi 5600 wa Daesh kutoka ktikia nchi 33 duniani warejea katika mataifa yao

Magaidi 5600 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh kutoka katika mataifa 33 ulimwenguni wamerudi katika mataifa yao, huku mataifa hayo yakiwa na mashaka yakuwa magaidi hao wanaweza wakafanya uharifu katika mataifa yao

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kushindwa nchini Iraq na Syria, kikundi hicho kwa sasa kimekuwa tishio kwa mataifa ya Ulaya na jamii zao.
Shirika la habari la SkyNews limetangaza katika habari yake kuwa magaidi 5600 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wakitoka katika mataifa 33 wamerejea katika mataifa yao, ambapo kuna mashaka makubwa ya kufanya matukio ya kigaidi katika mataifa hayo katika siku za usoni.
Mpaka sasa mataifa hayo hayajainisha njia ya kukabiliana na magaidi hao waliorudi kutoka nchini Iraq na Syria, ambapo asilimia kubwa kati yao hufungwa katika mataifa hayo huku wengine wakiishi kwa maficho katika nchi hizo.
Pia katika changamoto ziliopo katika mataifa hayo ni kuhusu watoto na familia za magaidi hao, kwa maana kuchanganyika familia hizo na familia zingine pia ni tatizo, kwani familia za magaidi ni watu ambao wameathirika kiseikolojia na mpaka sasa haijajulikana njia ya kuwasaidia watu hao haki upande wa watoto wa magaidi hao.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky