Magaidi 60 wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah wako nchini Ujeruman

Magaidi 60 wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah wako nchini Ujeruman

Jarida moja nchini Ujerumani limeeleza kuwepo kwa magaidi 60 wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusra nchini Ujerumani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jarida moja la kila wiki la Spiegel nchini Ujerumani katika moja ya ripoti zake limeelezea kuwepo kwa magaidi 60 wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah waliokuwa katika kikosi kinachoitwa (Uweisi Alqarni) ambao wameingia nchini humo kwa auani ya kuwa ni wakimbizi.
Kwa mujibu wa maelezo ya vyombo vya usalama vya Ujerumani, wanachama wa kikundi hicho cha kigaidi walishiriki katika matukio mengi ya mauaji ya wananchi wasiokuwa wanajeshi nchini Syria.
Aidha kikundi hicho awali kilikuwa chini ya kikundi kiitwacho jeshi huru la Syria na baada kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusra na kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia nchini humo.
Mpaka sasa serikali ya Ujerumani inafanya uchunguzi katika mafaili 25 ya magaidi hao, huku vyombo vya usalama nchini humo vinafuatili mafaili mengine ya magaidi wengine wa kikundi hicho waliopo hivi sasa nchini Ujerumani, ambapo wengine baadhi yao hawajafahamika ipasavyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky