Magaidi 8 wahukumiwa kunyongwa nchini Misri

Magaidi 8 wahukumiwa kunyongwa nchini Misri

Mahakama ya kijeshi nchini Misri imewahukumu magaidi 8 wa wilaya ya Sinai kunyongwa nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mahakama ya kijeshi nchini Misri imetoa hukumu ya kunyogwa watu 8 miongoni mwa magaidi wa wilaya ya Sinai ambao ni tawi lakikundi cha Daesh nchini, na wengine 32 katika magaidi kufungwa kifungo cha maisha.
Watu  hao wanatuhumiwa kwa kosa la kupanga mipango ya mashambulizi ya kigaidi na kuuwa wanajeshi 14 na raaia wa kawaida 16 katika matukio mbalimbali ya kigaidi nchini humo.
Watuhumiwa hao walitumia silaha mbalimbali ikiwemo makombora na miripuko mbalimbali iliotengezwa kienyeji nchini humo.
Maeneo mbalimbali ya sehemu ya jangwa la Sinai nchini Misri katika miaka kadhaa ya hivi mwishoni nchini humo yameonekana kutokea mashambulizi ya kigaidi dhidi ya majeshi ya nchi hiyo na wananchi wasiokuwa na hatia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky