Magaidi mmoja akamatwa nchini Singapore

Magaidi mmoja akamatwa nchini Singapore

Nchini Singapore akamatwa gaidi mmoja wa Daesh ambaye ni mwananchi wa Taifa hilo akituhumiwa kuwa katika juhudi za kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya ndani ya Singapore imetanganza kumkamata mwananchi mmoja wa nchi hiyo kwa tuhuma ya kufanya juhudi za kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchni Syria.
Kwa mujibu wa kauli ya wizara hii “Azah Zuhrah Ansariy” mwenye umri wa miaka 22 amekamatwa akiwa katika harakati za kusafiri kwenda nchini Syria pamoja na mtoto wake kwaajili ya kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo kwa mujibu wa wizara hiyo, kijana huyo daima alikuwa alikuwa akiunga mkonu vitengo wanavyo magaidi wa Daesh kwa njia ya mitandao ya kijamii.
Aidaha mwaka uliopita wananchi wawili wa Singapore walikamatwa kwa kosa la kusafiri kwenda nchini Syria kwaajili ya kutaka kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo, kwa upande mwingine jeshi la Polisi la Indonesia mwaka uliopita iliangamiza timu moja ya magaidi wa Daesh waliokuwa wanakusudia kufanya matukio ya kigaidi nchini Singapore.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh katika miaka ya hivi mwisho mara kadhaa wamefanya juhudi kubwa za kutaka kufanya mashambulio ya kigaidi katika nchi za Asia ya Mashariki kama vile Indonesia na Philipino.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky