Magaidi wa 690 kutoka Ufaransa wako nchini Iraq na Syria/ Ulaya yapata hofu kwa kurejea kwao

 Magaidi wa 690 kutoka Ufaransa wako nchini Iraq na Syria/ Ulaya yapata hofu kwa kurejea kwao

Wizara ya ulinzi na usalama ya Ufaransa imetoa habari yakuwa wafaransa 690 wapo na vikundi vya kigaidi nchini Syria na Iraq, huku viongozi hao wakiwa na hofu ya kutokea matukio ya kigaidi baada ya kurudi magaidi hao nchini humo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: baada ya wizara ya ulinzi na usalama ya Ufaransa yakuwa wananchi 690 wa nchi hiyo wako katika vikundi vya kigaidi nchini Iraq na Syria, viongozi wa nchi hiyo, viongozi wa nchini hiyo wanaumiza vichwa kwa hofu ya kutokea miripuko ya kigaidi watakaporudi magaidi hao nchini humo.
Televishen ya Ufaransa ya 24 imetangaza kuwa miongoni mwa magaidi 690 waliopo nchini Iraq na Syria magaidi 256 ni wanawake na 28 ni watoto wadogo.
Mkuu wa mahakama ya Ufaransa amesema kuhusu suala hilo, jambo hili hatuwezi kuliacha hivihivi tu kwa ni suala linalohusu amani na usalama wa taifa na jamii hiyo.
Aidha ameendelea kwa kusema kuwa: kurudi kwa magaidi hao nchini humo ni hatari kwa usalama wa nchi hasa kwa watoto na wanawake hao kwakuwa wamejifu jinsi ya kuathiri wengine.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky