Magaidi wa Boko Haram wafanya mauaji ya kinyama nchini Cameroon

Magaidi wa Boko Haram wafanya mauaji ya kinyama nchini Cameroon

Kwa mujibu wa ripoti ya `vyanzo vya habari nchini Cameroon ni kwamba kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kimefanya mauaji ya kigaidi katika maeneo ya kaskazini mwa mashariki mwa nchi hiyo ambayo ni sehemu inayopakana na Nigeria, ambapo wamefanya mashambulizi mawili ya kujirupua na kusababisha kuuwawa kwa watu 14 na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa

Shirika la habari  AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kimefanya mauaji ya kigaidi nchini Cameroon katika sehemu ya mipaka ya nchi hiyo na Nigeria.
Kwa mujibu wa ripoti ya vyanzo vya habari na vya usalama vya Cameroon, mashambulio hayo ya kigaidi kwa uchahc e yamepelekea kujeruhiwa watu zaidi ya 30 na kuuwawa watu 14 miongoni mwa wananchi wasiokuwa na hatia nchini humo.
Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kimefanya mashambulio mawili ya kujiripua katika moja ya maeneo yaliokuwa na msongamano mkubwa wa watu katika mji wa Waza, ambapo mabomu hayo katika migahawa na makao makuu ya simu na maduka ya wafanya biashara wadogowadogo kaskazini mwa mashari ya Cameroon.
Kwa mujibu wa taarifa ziliotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo ni kwamba hali ya majeruhi wa tukio hilo ni mbaya sana, ambapo miili yao imeharibiwa vibaya na miripoku hiyo.
Majeshi ya nchi hiyo yamezui kutoka na kuingia katika sehemu hiyo, ambapo haruhusiwi kuingia na kutoka yeyote, huku wakifanya juhudi za kufahamu chanzo na walioshiriki kufanya tukio hilo la kigaidi.
Tukio hilo limeto baada ya miezi kadhaa ya kuwepo utulivu nchini Cameroon, ambapo kikundi cha kigaidi cha Boko Haram na washirika wake kikundi cha Daesh nchini Afrika kufanya matukio mapywa ya kigaidi nchini humo.
Mpaka sasa kikundi cha Boko Haram nchini Cameroon kimesababisha watu laki mbili kuacha makazi yao katika maeneo ya kaskazini mwa mashariki mwa kutokana na kuhofia maisha yao na kwenda maeneo mengine mbalimbali kwaajili ya kuzinusuru roho zao.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky