Magaidi wa Daesh hawana pakukimbilia Iraq na Syria

Magaidi wa Daesh hawana pakukimbilia Iraq na Syria

: Vikosi vya Iraq vikisaidiwa na wataalamu wa kijeshi kutoka Iran vimeingia katika mji wa al-Qaim, moja ya maeneo yaliyokuwa yamesalia mikononi mwa kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Mafanikio kama hayo yanaripotiwa pia upande mwengine wa mpaka, yaani nchini Syria ambapo pia majeshi ya Iran yanatoa msaada wa karibu.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vikosi vya Iraq vikisaidiwa na wataalamu wa kijeshi kutoka Iran vimeingia katika mji wa al-Qaim, moja ya maeneo yaliyokuwa yamesalia mikononi mwa kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Mafanikio kama hayo yanaripotiwa pia upande mwengine wa mpaka, yaani nchini Syria ambapo pia majeshi ya Iran yanatoa msaada wa karibu.

Vikosi vya Iraq vimefanikiwa kuingia katika mji wa al-Qaim, ambao ni moja ya maeneo yaliyokuwa yamesalia mikononi mwa kundi la wanamgambo wanaojiita Dola la Kiislamu, IS na kuwazingira magaidi hao hatari wanaodhaminiwa na Saudia arabia.

Vikosi kutoka jeshi la Iraqi, Kikosi Maalum ya Kupambana na Ugaidi, vikiongozwa na wataalamu kutoka Iran, wanashiriki kwenye mashambulizi ya kuikomboa miji ya al-Qaim na Rawa, miji miwili ambayo iko katika eneo la mpaka wa Iraq na Syria. Meja Generali Noman Abed al-Zobai, aliongea na waandishi wa habari, kwamba vikosi hivyo vimekwishaanza mashambulizi katikati ya mji wa Al-Qaim.

Mapema asubuhi ya leo, majeshi ya Iraqi yalianzisha mashambulizi ya ardhini kwenye maeneo walikokuwa wanamgambo kundi la kigaidi la Daesh yakisaidiwa na wataalamu wa kijeshi kutoka Iran.

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, alisema kwenye taarifa yake iliyotangaza kuhusu operesheni hiyo wiki iliyopita kwamba "wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wanatakiwa kuchagua ama kufa au kusalimu amri."

Mafanikio makubwa yaonekana nchini Syria.

Wakati huo huo, jeshi la Syria limetangaza leo hii kwamba limeukomboa mji wenye utajiri wa mafuta ambao umepiganiwa kwa kipindi kirefu wa Deir el-Zour ulioko mashariki mwa nchi hiyo, kutoka kwa wanamgambo wa Dola la Kiislamu, hatua inayotajwa kama alama ya ushindi mkubwa katika operesheni za kijeshi za kukomboa ngome zilizosalia ambazo awali zilishikiliwa na kundi hilo katika jimbo lenye utajiri wa mafuta lililopo katika mpaka na Iraq na Syria.

Kwenye taarifa yake, jeshi la Syria limesema hivi sasa lina udhibiti kamili wa mji huo, baada ya kampeni ya wiki nzima iliyofanywa na vikosi vya Syria, Iran na Urusi. Limesema vikosi maalumu vya jeshi hivi sasa vinaondoa mitego na mabomu ya kufukiwa ardhini yaliyotegwa na wanamgambo kundi la kigaidi la Daesh katika mji huo.

Deir-el-Zour ilikuwa imegawika kwa takribani miaka mitatu, ambapo upande mmoja ulikuwa unashikiliwa na majeshi ya serikali na huku mwengine ukiwa chini ya utawala wa kundi la kigaidi la Daesh.

Majeshi ya serikali ya Syria kwa kushirikiana na majeshi washirika yanayounga mkono serikali hapo awali walifanikiwa kuliingia kwenye eneo lililokuwa limezingirwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh kwenye mji huo mnamo mwezi Septemba katika shambulizi lililopata usaidizi wa vikosi vya Urusi, na tangu hapo yamekuwa yakisonga mbele katika harakati za kuwafurusha wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake.

Hatua hii ni ya hivi karibuni inayoonesha kushindwa kwa kundi hilo la kigaidi linaloungwa mkono na marekani na washirika wake wa kiarabu, wakati wapiganaji hao wakishuhudia kunyang'anywa takriba ngome zote za mijini ambazo awali walijitangazia ukhalifa. 

Jeshi la Syria, linaloungwa mkono na Urusi na Iran, hivi sasa vinasonga mbele kuikomboa miji iliyosalia katika jimbo la mashariki lenye utajiri wa mafuta, ukiwemo mji muhimu wa Boukamal, uliopo karibu na mpaka wa Iraq.    

Mwisho wa habari / 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky