Magaidi wa Daesh waendelea kukipata chamtema kuni Syria

Magaidi wa Daesh waendelea kukipata chamtema kuni Syria

Magaidi wa kundi la Daesh ambao wanamafungamano ya karibu na Saudia Arabia na Uturuki wameendelea kukimbia maeneo mbalimbali ya Syria baada ya jeshi la serikali kushadidisha mashambulizi dhidi ya magaidi hao hatari.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Magaidi wa kundi la Daesh ambao wanamafungamano ya karibu na Saudia Arabia na Uturuki wameendelea kukimbia maeneo mbalimbali ya Syria baada ya jeshi la serikali kushadidisha mashambulizi dhidi ya magaidi hao hatari.

Maelfu ya raia wa Syria wameyakimbia mapigano makali kati ya vikosi vya serikali  vinayoungwa mkono na Urusi na Iran dhidi ya  wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.

Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa na mashambulizi ya anga na mizinga ya Urusi na Iran vimeendesha mapambano makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh na kuvikomboa takriban vijiji 80 viliokuwa kwenye mikono ya wapiganaji hao wanaopata udhamini kutoka kwa Saudia Arabia, Marekani na Uturuki.

Kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria lengo la mashambulizi ya vikosi vya serikali ni kuukomboa mji wa Kahafsah unaoshikiliwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh ambao una kituo kikuu chenye kusambaza maji kwa mji wa Allepo.

Wakazi katika mji wa Allepo ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria wamekuwa hawapati huduma ya maji kwa siku 47 baada ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh kukata usambazaji wa maji kwa mji huo .Mapigano hayo katika kipindi cha wiki moja yamesababisha wimbi la zaidi ya raia 30,000 kukimbia wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

Wengi wakimbilia mji wa Manbij

Mkuu wa shirika hilo Rami Abdel-Rahman amesema wengi ya watu waliokimbia mapigano hayo wamekwenda kwenye maeneo karibu na mji wa Manbij unaodhibitiwa na vikosi vya (SDF) washirika wa wapiganaji wa Kikudi na Waarabu wanaoungwa mkono na Marekani ambayo yanatumiwa kupambana na majeshi ya serikali.

Wengi wao wameshuhudiwa wakielekea katika mji huo kwa kutumia piki piki,mabasi madogo na magari na wengi wao wameonekana kuwa wachovu wakiwa katika misururu kwenye kituo cha ukaguzi kwa jili ya kupekuliwa na kupata ruhusa ya kuingia.

Ibrahim al-Quftan mwenyekiti mwenza wa mamlaka ya kiraia ya mji wa Manbij na waandishi wa habari kwamba takriban watu 40,000 wamewasili katika mji huo katika siku za hivi karibuni. Ameongeza kusema idadi hiyo ya watu waliopotezewa makazi inaendelea kuongezeka kutokana na mapigano kati ya majeshi ya serikali ya Syria na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.

Na kwa mujibu wa Abdel Rahman wa shirika la haki za binaadamu nchini Syria mji huo wa Manbij tayari unawapa hifadhi maelfu ya watu waliopotezewa makazi ambao waliyakimbia mapigano yaliyopita katika eneo hilo na wanaishi katika mazingira magumu. Amesema hali hiyo itafanya iwe vigumu kwa mamlaka ya mji huo kukaribisha wimbi jipya la watu waliopotezewa makaazi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kushughulikia mahitaji yao ya msingi.

Vita vinavyochochewa na magaidi wanaotumwa na Marekani na washirika wake vilianza nchini Syria hapo mwezi wa Machi mwaka 2011 zaidi ya nusu ya idadi ya watu wake kabla ya vita hivyo kuanza wamelazimika kuyakimbia makazi yao. Mkoa wa kaskazini wa Aleppo una maelfu ya Wasyria waliopotezewa makazi wengi wao wakiwa katika makambi na mpaka na Uturuki.

Zaidi ya watu 310,000 wameuwawa tokea magaidi wanaotumwa na Marekani waanze kushambulia na kuteka miji ya Syria.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky