Magaidi wa Daesh waukimbia mji wa Alqaim kwenda nchini Syria

Magaidi wa Daesh waukimbia mji wa Alqaim kwenda nchini Syria

Vyombo vya habari nchini Iraq vimetangaza kuwa makundi ya magaidi wa Daesh katika mji wa Alqaim nchini Iraq wameweka silaha zao chini na kukimbilia mji mmoja uliopo mchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari nchini Iraq vimetangaza kuwa magaidi wa kikundi cha Daesh walikuwa katika mji wa Qaim nchini Iraq wameweka silaha zao chini na kukimbilia mji wa Bokamali katika mipaka ya Syria na Iraq.
Kukimbia kwa kikundi cha Daesh katika mji wa Qaim, imetokea baada ya majeshi ya Iraq na ndege zao za kivita kushambulia sehemu za magaidi hao na kuangamia asilimia kubwa ya magaidi hao kufuatia shambulio hilo.
Kabla ya hapo kikundi cha kigaidi cha Daesh sehemu hiyo kilitoa tangazo na kufikishiwa wananchi wote kuwa mtu yeyote hapaswi kuondoka katika sehemu hiyo na yeyote atakayeamua kikimbia atahesabiwa kuwa ni muahini na watapewa adhabu kali.
Inasemekana kwamba majeshi ya Iraq katika masiku kadhaa yaliopita yalianza mashambulizi makali yakilenga kuukomboa mji wa Al-qaim na maeneo yaliopakana na Syria ambapo ndio maeneo ya mwisho yaliopo vikundi vya kigaidi vya Daesh katika ardhi ya Iraq.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky