Magaidi waalazimia kuwaacha huru wafungwa baada ya kuzidiwa nchini Iraq

Magaidi waalazimia  kuwaacha huru wafungwa baada ya kuzidiwa nchini Iraq

kundi la kigaidi la Daesh limewaachia huru wafungwa kadhaa waliokuwa wamewazuia kwenye jela

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: kundi la kigaidi la Daesh limewaachia huru wafungwa kadhaa waliokuwa wamewazuia kwenye jela za wilaya ya kaskazini mwa mji wa Mosul ambazo bado zinashikiliwa na kundi hilo la kigaidi linalodhaminiwa na muungano wa nchi za kiarabu na Magharibi. Hata hivyo hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya kundi hilo la kigaidi la Daesh kuendelea kushindwa nguvu na vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na  wataalamu wa masuala ya kijeshi kutoka Iran.

Vikosi vya serikali ya Iraq vilianzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Mosul tangu Oktoba mwaka jana. Mosul ni ngome ya mwisho ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq. Miongoni mwa watu walioachiwa ni wale waliokamatwa wakiuza sigara na walihukumiwa kwa kukiuka marufuku ya uvutaji sigara wengine walikamatwa kwa kukutwa na simu za mkononi ambazo ilihofiwa huenda walizitumia kuwasiliana na ulimwengu wa nje. Zaidu ya Nusu ya mji wa Mosul tayari umeshakombolewa kutoka kwa magaidi hao.  kundi la kigaidi la Daesh limeondolewa kwenye miji mingi waliyoiteka kati ya mwaka 2014 n1 2015.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky