Magaidi wanaodhamiwa na Marekani washambulia vikosi vya Syria

Magaidi wanaodhamiwa na Marekani washambulia vikosi vya Syria

Majeshi ya magaidi yanayoongozwa na Marekani katika kupambana na serikali ya Syria yamefanya mashambulizi ya anga dhidi ya vikosi vinavyomuunga mkono rais wa Syria Bashar al Assad.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Majeshi ya magaidi yanayoongozwa na Marekani  katika kupambana na serikali ya Syria yamefanya mashambulizi ya anga  dhidi ya vikosi vinavyomuunga mkono rais wa Syria Bashar al Assad.

Muungano wa majeshi ya magaidi yanayoongozwa na Marekani  katika kupambana ili kuitoa serikali ya Syria madarakani umefanya mashambulizi ya anga  dhidi ya vikosi vinavyomuunga mkono rais wa Syria Bashar al Assad na kuwaua zaidi ya wapiganaji 100 wa vikosi vya serikali. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Marekani.  Mashambulizi hayo ya anga yalikuwa yanalenga kujibu shambulizi lilofanywa  katika makao makuu  ya vikosi washirika na Marekani vya Syrian Demokrasia Forces  (SDF) na kuwaua mamia ya wanajeshi wa mataifa mbalimali ikiwemo Marekani ambao walikuwa wakitoa misaada na mafunzo kwa magaidi hao.

 Afisa mmoja wa  jeshi la Marekani amesema wanakisia kuwa zaidi ya wapiganaji 100 wa vikosi vinavyounga mkono utawala wa  Syria wameuawa wakati wa mashambulizi hayo ya makombora ya kushtukiza.

Shambulizi lilikuwa kali sana

Amesema shambulizi hilo lililoanza jana Jumatano   lilihusisha wapiganaji 500 wa vikosi  vinavyoiunga mkono serikali ya Syria vilivyokuwa vikitumia vifaru na silaha nyingine katika mapambano dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani.

Hata hivyo afisa huyo wa jeshi la Marekani hakufafanua zaidi iwapo vikosi ambavyo vilikuwa vinapambana na muungano na majeshi yanayoongozwa na Marekani vilikuwa ni vya serikali ya Syria au vya makundi  kadhaa  ya  wanamgambo washirika  yakiwemo kutoka Iraq na Lebanon,  ambayo yamekuwa yakimuunga mkono rais Assad tangu mapigano ya yanayochochewa na Marekani yalipozuka nchini Syria miaka saba iliyopita.

Urusi nayo pia imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga mazito nchini humo kumuunga mkono rais Bashar Assad ambaye pia amekuwa akisaidiwa  na makomandoo kutoka Iran.

Kundi la magaidi wa SDF ambao ni muungano wa vikosi vya Kikurdi na wapiganaji wa makundi ya kigaidi  linashirikiana na vikosi vya muungano wan chi 61 unaooongozwa na Marekani  katika juhudi zilizogonga mwamba za kuiangusha serikali ya Syria.

Shambulizi hilo linaweza kusababisha changamoto zaidi  kwa wapiganaji wa vikosi vya magaidi vinavyoungwa mkono na Marekani  ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakijaribu kuhakikisha wanasonga mbele dhidi ya vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya rais Bashar Assad.

Wakati huohuo kwa mjibu wa Ikulu ya Urusi Kremlin rais Vladimir Putin na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan  wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye operesheni za kijeshi na kiusalama nchini Syria katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Katika mazungumzo yao kwa njia ya simu rais Putin na Erdogan walijadili pia juu ya kuwa na mawasiliano mapya yatakayoijumuisha pia Iran kujadili mgogoro huo wa Syria na kwa mujibu  wa Kremlin viongozi hao pia walijadili juu ya haja ya kufanyika mkutano huo wa kilele kati ya viongozi wa nchi hizo tatu ingawa tarehe haijapangwa.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky