Magaidi wanaongwa mkono na Uturuki waingia katika makao makuu ya mji wa Al-bab nchini Syria+ picha

 Magaidi wanaongwa mkono na Uturuki waingia katika makao makuu ya mji wa Al-bab nchini Syria+ picha

Rais wa serikali ya Uturuki amesema kuwa: hali halisi ya sehemu ya Al-bab iko katika kuzingirwa na majeshi yake yakishirikiana na majeshi ya waasi wasliokuwa dhidi ya Syria, ambapo kikundi cha kigaidi cha Daesh kimeanza kuondoka sehemu hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rajab Tayyip Erdogan, Rais wa jamhuri ya Uturuki amesema kuwa majeshi ya taifa lake wakishirikiana na waasi wa serikali ya Syria wamewasili katika makao makuu ya mji wa Al-bab kaskazini mwa Syria.
Mji huo umemilikiwa na magaidi wa Daesh, amabapo waasi wanaoipinga serikali ya Syria wameungana na kusaidiwa na majeshi ya Uturuki kwaajili ya kuiteka sehemu hiyo, ambapo mwezi uliopita walianza kufanya mashambulio makubwa dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh kwaajili kuuteka mji wa Al-bab nchini humo.
Rajab Tayyip Erdogan amesema: mji wa Al-bab umezingirwa na majeshi ya nchi yetu yakishirikiana na waasi walio dhidi ya serikali ya Rais wa Syria, huku magaidi wa Daesh waliopo sehemu hiyo wamenza kuondoka sehemu hiyo.
Mji wa Al-bab ndio sehemu ya mwisho iliokuwa na kambi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mkoa wa Aleepo nchini Syria.
Rais wa Uturuki amesema; malengo ya kuwepo majeshi ya Uturuki nchini Syria ni kile alichokitaja kuwa ni kuvisambaratisha vikundi vya kigaidi nchini humo katika sehemu iliokuwa na umbali wa kilometa elfu 5 mpaka kufika katika mji wa Raqqeh nchini Syria.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky