Magaidi wawili wa Daesh wakamatwa nchini Ispania

Magaidi wawili wa Daesh wakamatwa nchini Ispania

Wizara ya mambo ya ndani ya Ispania imetangaza kukamtwa kwa watu wawili kwa tuhuma ya kuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuwa wanasajili watu kwaajili ya kujiunga na kikundi hicho cha kigaidi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kukamatwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh zatangazwa nchini Ispania
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo  imetangaza kukamata mtu mmoja aliokuwa na uraia wa Misri na mwingine akiwa ni mwananchi wa Ispania, kwa tuhumu yakuwa wanamahusiano na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hii ni kwamba apo awali alikamtwa mke wa Muispania huyo kwa tuhuma ya kushawishi watu kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh ikiwemo kusajili watu kwaajili ya kujiunga na kikundi hicho cha kigaidi nchini humo.
Aidha Jeshi la Polisi la Ispania limetangaza limekamata watu wanane ambao asilimia kubwa ni raia wa Morocco wakituhumiwa na makosa ya kuwa na mawasiliano na vikundi vya kigaidi viliokuwa na sila na kushiriki katika mauaji mbalimbali katika mji wa Barcelona kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikundi cha kigaid cha Daesh katika miaka ya hivi mwishoni kimefanya mashambulizi ya kigadi katika nchi mbalimbali za Ulaya ikiwemo Ufaransa, Ujerumani na  Belgium, ambapo mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya mamia ya wananchi wa na wengine kujeruhiwa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky