Mahaka ya kijeshi ya Pakistan yanyonga magaidi watatu

Mahaka ya kijeshi ya Pakistan yanyonga magaidi watatu

Jeshi la Pakistan limetangaza kunyongwa kwa magaidi watatu wanaofungamana na kikundi cha kigaidi cha (Harakatul Jihadi) na kikundi cha (Tahrik Taliban Pakistan) nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: magaidi watatu wa vikundi vya kigaidi nchini Pakistani wamenyongwa nchini humo.
Magaidi hao walijihusika kufanya matukio ya kigaidi mbalimbali nchini humo, ikiwemo kushambulia majeshi ya usalama wa nchi hiyo, kushambulia wananchi wa kawaida, kushambulia vituo mbalimbali katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Kunyongwa kwa magaidi hao, kumefuatia hukumu iliotolewa na mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo, ambapo hukumu hiyo ilitolewa katika hali ambayo, mahakama hiyo imeongezewa muda wa kufanya harakati zake nchini humo, ambapo maamuzi ya kuongezewa muda huo yamemeonekana kupingwa na wananchi wa nchi hiyo, ambapo asilimia kubwa ya vyama vya nchi hiyo vimepinga kiendelea kwa harakati za mahakama hiyo, huku vyama vingine vikiunga mkono kuendelea kwa harakati za Mahakam hiyo ya kijeshi.
Aidha Jumatano ya wiki iliopita jeshi la nchi hiyo, lilitoa hukumu ya kunyongwa kwa magaidi watano wa kikundi cha kigaidi cha Taleban nchini Pakistan waliopo katika jela ya mji wa Kuhat nchini humo.
Jeshi la serikali ya Pakistan limesema kuwa: mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo, kwa muda wa miaka miwili ya harakati zake mpaka sasa, zimetoa hukumu za kinyongo kwa magaidi 161 wa vikundi vya kigaidi viliopo nchini humo ambapo mpaka sasa magaidi 21 walishanyongwa kufuatia hukumu hizo.
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky