Mahakama kuu ya Nigeria yaitaka serikali kumuacha huru sheikh Zakizakiy

Mahakama kuu ya Nigeria yaitaka serikali kumuacha huru sheikh Zakizakiy

Msimamizi wa mahakama kuu ya Nigeria ameitaka serikali ya nchi hiyo kufuata katiba ya nchi hiyo na kumuachia huru Sheikh Zakizakiy “kiongozi wa harakati ya Kiislamu Nigeria” haraka iwezekanavyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mkuu wa mahakama kuu ya Nigeria aliochaguliwa katika nafasi hiyo hivi karibuni, amegusia suala la Sheikh Ibrahim Zakizakiy “kiongozi wa harakati ya Kiislamu Nigeria” na kuitaka serikali ya nchini hiyo kumuacha huru sheikh huyo haraka iwezekanavyo.
Akisisitiza suala hilo mkuu wa mahakama kuu ya Nigeria amesema: vyombo vya kisheria vinapaswa kuwa huru kutoka kwa mashinikizo ya serikali zao, huku akiitaka serikali ya Nigeria kutekeleza hukumu iliotolea na mahakama ya nchi hiyo hiyo.
Rais na mkuu wa mahakama kuu ya Nigeria, aliyeapishwa kwa kusimamia mahakama hiyo hivi karibuni amesema: serikali ya Muhammad Buhari, kwa kuacha kufuata na kutekeleza hukumu zinazotolewa na mahakama hiyo, khususan kuhusu kuachiwa huru Sheikh Zakizakiy “ kiongozi mkuu wa harakati ya kiislamu Nigeria” maana yake ni kuto zingatia na kuheshimu maamuzi ya mahakama hiyo na kuporwa nafasi yake nchini humo, ambapo hukumu zake kuonekana kama makaratizi yasiokuwa na thamani yeyote.
Hakimu mkuu wa mahakama hiyo aliendelea kuashiria kwa kusema: kukithi kwa wimbi la kukosolewa kwa serikali ya Nigeria vhini ya Rais “Muhammad Buhari” msingi wake unatokana na kuto fuata na kupuuza kufuata katiba na sheria za nchi hiyo.
Wito huu umetokea baada ya kupita miezi mene ya mahakama kuu ya nchi hiyo kutoa hukumu ya kuachiwa huru kiongozi wa harakati ya Kiislamu Nigeria “sheikh Ibrahim Zakizakiy” na mke wake, ambapo mahakama hiyo ilithibitisha kuwa kiongizi huyo na familia yake hana kosa na hakuwa mwenye kukiuka sheria za nchi hiyo, hivyo mahakama hiyo kuitaka serikali ya Nigeria kumuacha huru kiongozi huyo ndani ya muda wa siku 45 na kuwalipa kiwango fulani cha pesa kutokana na usumbufu aliopata kiongozi huyo na mke wake, ama baada ya kupita zaidi ya miezi miwili ya muda ulioanishwa wa kumuacha huru shrikh huyo, serikali ya Nigeria mpaka sasa bado haijatekeleza hukumu hiyo iliotolewa na mahakama hiyo.
mwisho wa habari/ 290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky