Majeshi ya Iraq yagundua kituo cha mafunzo ya kigaidi katika maanda ya 10 kwenda chini+ picha

Majeshi ya Iraq yagundua kituo cha mafunzo ya kigaidi katika maanda ya 10 kwenda chini+ picha

vikosi vya majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuyakomboa maeneo makubwa ya upande wa magharibi mwa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuwaondoa katika maeneo hayo

shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Iraq yamegundua andaki liliokuwa na urefu wa mita 10 kwenda chini, ambayo yamechimbwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh kusini mwa mji wa Musol.
Magaid wa Daesh walikuwa wakitumia maandaki hayo kwaajili ya kufundisha ugaidi kwa magaidi wa mataifa mbalimbali katika sehemu hiyo, huku wakisisitiza mlango wa maingilio ya maandaki hayo, ni mdogo kiasi kwamba lazima  uingie kwa kukwawa kwa kutumia kifua.
Mmoja kati ya makamanda wa majeshi ya Iraq amesema: moja kati ya ratiba za mafunzo ya kikundi cha kigaidi cha Daesh ni mafunzo ya kukwawa kwa kifua, ambapo baada ya kupita katika hatua hiyo ndipo magaidi waliopo katika mafunzo hayo wanaruhusiwa kuanza hatua nyingine ya mafunzo mengine ya kikundi hicho.
Aidha ameongeza kuesema kuwa maandaki hayo yamechipwa na kujengwa vizuri bila ya mapungufu yeyote, ambao kwamba ni ujenzi wa kisasa zaidi kuhusu taaluma ya utengezaji maandaki uliompo ulimwenguni, ambapo sehemu hiyo ndio ilikuwa sehemu maalumu ya kufunzwa ugaidi kwa magaidi wanaotokea mataifa ya kigeni nchini humo.
Kwa mujibu wa  maelezo ya wakazi wa sehemu hiyo ni kwamba; majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuikomboa sehemu ya kubwa ya kusini mwa mji wa Musol, siku ya Jumatano ya tarehe moja mwezi Machi, na kuvisambaratisha vikundi vya kigaidi vya Daesh katika sehemu hizo.
Jenerali mmoja wa majeshi ya Iraq amesema kuwa majeshi ya Iraq baada ya mapambano makali yamefanikiwa kukomboa sehemu hizo, na wamefanikiwa kufika katika mlango mkuu wa kuingia Syria kupitia Musol kwa umbali wa kilometa 2 kaskazini mwa magharibi mwa Musol.
Barabara ya Musol kwenda Tal Afar ni sehemu nyingine muhimu za maficho ya kikundi cha kigaidi cha Daesh magharibi mwa Musol, ambayo inaungana na nchi ya Syria.
Viongozi wa Iraq walitoa amri ya kuanza hatua za kuukomboa mji wa Musol toka tarehe 16 mwezi Octoba mwaka jana ambapo walisema kuwa: mji wa Musol unamagaidi wa Daesh wapatao elfu sita, ambapo kwa mujibu wa maelezo ya makanda wa majeshi ya Iraq ni kwamba kufuatia mashambulizi ya kuikomboa sehemu ya Humeh ya mashariki ya Musol, kwa uchache magaidi elfu tatu na miatatu wameangamia katika mashambulio hayo.
Majeshi ya usalama ya Iraq yalianza mashambulizi ya kuyakomboa maeneo ya magaharibi mwa Musol tarehe 19 mwezi wa pili mwaka huu na kushiriki mashambulio hayo maelfu ya majeshi ya nchi hiyo wakishirikiana na majeshi ya wananchi waliojitolea katika kupambana na magaidi nchini humo.
Mji wa Musol ndio makao makuu ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq ambapo ulitekwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh mnamo mwezi Juni mwaka 2014 nchini humo.

mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky