Majeshi ya Iraq yaingia sehemu ya Al-ayadhiyah katika mji wa Tal Afar

Majeshi ya Iraq yaingia sehemu ya Al-ayadhiyah katika mji wa Tal Afar

Majeshi ya serikali ya Iraq jana siku ya Jumatatu yamewasili katika sehemu ya Al-ayadhiyah iliopo pempezoni mwa mji wa Tal Afar nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Iraq kwa ushirikiano wa vikosi vyote, ikiwemo majeshi ya Polisi na vikundi vya wananchi waliojitolea katika kukabiliana na ugaidi nchini humo, wamewasili katika sehemu ya Al-ayadhiyah iliopo pembeni mwa mji wa Tal Far.
Vyanzo vya habari nchini humo vimetangaza kuwa vikosi 16 vya majeshi ya nchi hiyo, wamefanikiwa kuingia sehemu hiyo baada ya mapambano makali baina majeshi hayo na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Majeshi ya Iraq siku ya Jumapili yalifanikiwa kuukomoa mji wa Tal Afar, huku kikundi cha kigaidi cha Daesh kikimbilia sehemu ya Al-aayadhiyah iliopo pemeni mwa Tal Afar pamoja na vijiji vilio izunguka Al-ayadhiaya, ambapo majeshi ya Iraq baada mashambulizi makili pia yamefanikiwa kuingia sehemu hiyo ya Al-ayadhiya, hatimaye kukamilisha rasmi kumaliza kuikomboa Tal Afar na sehemu zake zinayoizunguka sehemu hiyo.
mwisho/ 290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky