Majeshi ya Iraq yakamisha maandalizi ya kufanya mashambulizi ya kuikomboa Tal Afar nchini Iraq

Majeshi ya Iraq yakamisha maandalizi ya kufanya mashambulizi ya kuikomboa Tal Afar nchini Iraq

Wizara ya ulinzi na usalama nchini Iraq imeeleza kukamilika kwa maandalizi ya jeshi lake kwaajili ya kuanza mashambulizi makali ya kuukomboa mji wa Tal Afar uliopo magharibi mwa Musol nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi na usalama nchini Iraq imeeleza kuwa jeshi lake limejianda kikamilifu kwaajili ya kuanza mashambulizi makali ya kuikomboa Tal Afar iliopo magharibi mwa Musol nchini Iraq.

Aidha msemaji wa wizara ya ulinzi na usalama nchini humo amesema kuwa: majeshi ya ulinzi na usalama ya nchi hiyo yamekamata makumi ya magaidi ya Daesh waliokuwa wamekimbia katika mji wa Musol, ambao walikuwa wamejichanganya na wananchi wa kawaida.

Inasemekana kuwa Fuadi Maasum Rais wa jamhuri ya Iraq wiki iliopita ametangaza kukamilika kwa maandalizi ya wanajeshi wa nchi hiyo kwa ukamilifu kwaajili ya kuanza mashambulizi ya kuikomboa Tal Afar, Alhuwaijeh na baadhi ya miji iliokuwa chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky