Majeshi ya Iraq yakomboa vijiji 150 na kuangamiza magaidi 385 katika mashambulizi ya kuikomboa Hawija

Majeshi ya Iraq yakomboa vijiji 150 na kuangamiza magaidi 385 katika mashambulizi ya kuikomboa Hawija

Kamanda wa mashambulizi ya kuikomboa Hawija ameelezea hatua walioifikia katika kuikomboa sehemu hiyo nakusisitiza kuwa wamefanikiwa kukomboa vijiji 150 na kuwaangamiza magaidi wa Daesh 385

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda wa mashambulizi ya kuikomboa sehemu ya Hawija amesema kuwa majeshi ya Iraq yamefanikiwa kukomboa vijiji 150 na wamefanikiwa kuwasambaratisha magaidi 385 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ikiwa ni katika mafainikio ya mashambulio hayo.
Aidha “Abdulamiri Rashidi Yrallah” aendelea kubainisha kuwa: wamrfanikiwa kuangamiza magari 95 yaliokuwa yametegwa mabomu na kutegua mabomu 422 yaliokuwa yametegwa sehemu mbalimbali, pia wamesambaratisha sehemu 20 za maficho ya magaidi hao na viwanda vitano vya kuzalisha silaha.
Aliendelea kusema kuwa; katika sehemu hizo wameteka silaha nyingi sana, huku wakiangamiza sehemu 25 za kujikinga na vita, barabara 10 za chini ya ardhi, ghala 10 za silaha na sehemu 5 za kuripoti habari nchini humo.
Kwa upande mwingine vyombo vya habari vya mkoa wa Kirkuk nchini Iraq leo vimetangaza kuangamia kwa gaidi “Abu Aabdillah Atajikiy” ambaye kiongozi wa mafunzo ya snaipa katika kikundi cha kigaidi cha Daesh akiwa pamoja na baadhi ya magaidi wengine nchini humo.
Kwakuikomboa sehemu ya Hawija, serikali ya Iraq itakuwa imefanikiwa kuwaondoa magaidi wa Daesh katika ardhi za nchi hiyo, ambapo yatabaki maeneo machache tu yanayopakana na Syria ndio yatakayokuwa na magaidi hao.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky