Majeshi ya Israel yashambulia Syria

Majeshi ya Israel yashambulia Syria

Majeshi ya Iran kwasasa yapo nchini Syria na yanaendelea na kazi za kuyaangamiza makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, Israel na washirika wao, uwepo wa majeshi ya Iran nchini Syria ni hatari kubwa kwa usalama wa Israel.
Majeshi ya Iran yamesema yatazisaidia Syria, Palestina na Lebanon kurudisha ardhi zao na kupambana na Israel mpaka mwisho wa taifa la Israel.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Israel imeshambulia  maeneo ndani  ya  ardhi  ya Syria mara tatu  mapema leo Jumanne kwa  ndege  za  kivita pamoja  na  makombora na mizinga , limesema  jeshi  la  Syria katika taarifa  iliyotangazwa  na  televisheni  ya  taifa.

Ndege  za  jeshi la Israel  zimeshambulia  eneo  la Qutayfeh  kaskazini  mashariki  mwa  mji  mkuu  Damascus , na  makombora  yaliangukia  karibu  na  maeneo  ya kijeshi  na  kusababisha  jeshi  la  Syria kujibu mashambulizi na kuijeruhi ndege ya kivita ya Israel.

Israel  pia  ilifanya  mashambulio  ya  makombora  ya ardhini  ndani  ya  Syria  kutoka  katika  eneo  linalokaliwa na  Israel  la  milima  ya  Golan, lakini  jeshi  la  Syria limeyazuia makombora  hayo, na kushambulia vikali kambi za jeshi za Israel.

Taarifa  ilisema  kwamba  ndege  za  jeshi  la  Israel baada ya kushindwa kuingia Syria zilishambulia  tena  kwa  mara ya  mwisho kwa maroketi manne  kutoka  ndani  ya  Israel, na  kwamba mfumo  wa ulinzi  wa  anga  wa  Syria  ulifanikiwa  kuangusha  baadhi ya  makombora  hayo.

Jeshi  la  Syria limesema mfumo wa kulinda  anga umefanikiwa  kuangusha  baaadhi  ya  makombora  hayo na mengine  yaliangukia  katika  moja  kati  ya  maeneo  ya kijeshi  ya  syria, na  kusababisha  uharibifu  wa  mali.

Mwisho wa uchokozi wa Israel umewadia

Jeshi  la  Israel  limekuwa  likifanya  mashambulizi  mara kwa mara  dhidi  ya  jeshi  la  Syria  na  washirika  wake  wa Lebanon, wa  kundi  la  Washia  la  Hezbollah  tangu mwanzo  wa  mzozo  wa  ndani  wa  Syria  mwaka  2011. Ambapo jeshi la Israel limekuwa likiyasaidia makundi ya kigaidi yanayopambana na serikali ya Syria.

Msemaji  wa  jeshi  la  Israel  alikataa  kuelezea  lolote kuhusiana  na  taarifa  iliyotolewa  na  Syria. Licha  ya kuwa  mkuu  wa  jeshi  la  Israel  mwezi  Agosti  mwaka jana  alisema  kwamba  wanajeshi  wake  waliishambulia Syria  karibu  mara  100, sera  za  Israel  kwa  jumla  ni kutothibitisha  ama  kukataa  operesheni  kama  hizo.

Israel  imeapa kuizuwia Iran  kutumia  ardhi  ya  Syria kuweka  vituo vyake  vya  kijeshi  ama  kupitishia  silaha nzito  kwenda  kwa  kundi  la  Hezbollah  nchini  Lebanon, kundi  ambalo  limekuwa likisaidia  Syria  katika  vita  vyake dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekanina washirka wake vilivyodumu kwa miaka saba huku jeshi la Syria likionyesha mafanikio.

Katika  taarifa  yake  jeshi la  Syria imetoa  onyo  kabla  la  kulipiza  kisasi  kwa  mashambulizi  hayo ya  anga  na  kubainisha kuwa Israel inaendelea kuyasaidia makundi yakigaidi nchini Syria.  maba

Israel  ilikamata  kilometa  1,200  za  milima  ya  Golan kutoka  Syria  katika  vita  vya  siku  sita  vya  mwaka  1967 na  baadaye  kulichukua  kabisa  eneo  hilo  katika  hatua ambayo  haijatambuliwa na  jumuiya  ya  kimataifa. Syria na  Israel  zinaendelea  kuwa  katika  hali  ya  kivita, na taifa  hilo  la  Kiyahudi  lilipigana  vita  vikali dhidi  ya Hezbollah  mwaka  2006 ambapo majeshi ya Israel yalilazimika kusalimu amri kwa mara ya kwanza.

Majeshi ya Iran kwasasa yapo nchini Syria na yanaendelea na kazi za kuyaangamiza makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, Israel na washirika wao, uwepo wa majeshi ya Iran nchini Syria ni hatari kubwa kwa usalama wa Israel.

Majeshi ya Iran yamesema yatazisaidia Syria, Palestina na Lebanon kurudisha ardhi zao na kupambana na Israel mpaka mwisho wa taifa la Israel.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky