Majeshi ya Sudan yapata kipigo kikali nchini Yemen

Majeshi ya Sudan yapata kipigo kikali nchini Yemen

Msemaji mkuu wa majeshi ya Yemen ametangaza kufanikiwa kwao kutoa kipigo kikali dhidi ya majeshi ya Sudani katika ufukwe wa magharibi ya nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Yahya Sariu “ambaye ni msemaji mkuu wa majeshi ya Yemen” katika mji mkuu wa Sana`a na kutoa ripoti ya kuwaangamiza wanajeshi 25 kutoka nchini Sudan, ambapo majeshi ya Sudan yalikuwa katika juhudi za kutaka kuyamiliki maeneo yaliopo katika ufukwe wa magaharibi mwa Yemen.
Aidha akiendelea kubainisha sua;la hilo amesema: wanajeshi zaidi ya 200 wa majeshi ya umoja wa kivamizi unaosimamiwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, wamekufa na kujeruhiwa, ambapo asubuhi ya leo maiti za wanajeshi 28 zimeshafikishwa katika Hospitali ya Alkhukhah nchini humo.
Mwisho amemaliza kwa kusema kuwa wamefanikiwa kuteka kundi la mamluki wa Abdrabbuh Mansur Hadi, Rais wa Yemen aliokuwa amejiuzulu, huku akisisitisha kuzisambaratisha gari 19 za mamluki hao kupitia majeshi ya Yemen.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky