Majeshi ya Syria yasonga mbele dhidi ya magaidi wa Daesh

Majeshi ya Syria yasonga mbele dhidi ya magaidi wa Daesh

Majeshi ya serikali ya Syria yamefanikiwa kukikomboa kisima cha gesi cha “Hayani” na mitambo yake katika sehemu ya Humeh ya mashariki mwa mkoa wa Homs kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh

Shirika la AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Syria yamefikia ushindi huo leo siku ya Jumanne katika mkoa wa Homs nchini Syria, ambapo majeshi hayo yamekikomboa kisima hicho na kiwanda hicho cha kuzalisha gesi hiyo katika mkoa wa Homs nchini Syria.
Mpaka hivi sasa majeshi ya Syria yapo katika harakati ya kusafisha maeneo yalio kombolewa ikiwemo kutegua mabomu yaliotegwa na magaidi hao.
Wiki kadha ziliopita magaidi wa kikundi cha Daesh waliripua baadhi ya vitendea kazi vya kuzalisha gesi, ikiwemo kuripua bomba la kusafirisha gesi katika sehemu hiyo.
Wizara ya ulinzi ya Urusi jana imetangaza kuwa majeshi ya Syria yamesonga mbele kuelekea mji wa Palmyra. Huku wakisistiza kwamba majeshi ya Syria kwa muda wa wiki moja wameweza kusonga mbele kwa umbali wa kilometa 20 za mraba na kufika pembezoni mwa mji wa Palmyra na kuimiliki sehemu hiyo kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Mji wa Palmyra ni miungoni mwa miji ya kihistoria uliopo sehemu ya Humeh ya mashariki mwa mkoa wa Palmyra ambapo mnamo mwezi Desemba mwaka jana uliingia mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.      
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky