Majeshi ya Syria yavunja mzingiro wa waasi

Majeshi ya Syria yavunja mzingiro wa waasi

Jeshi la Syria limevunja mzingiro uliokuwa umewekwa na waasi kuizunguka kambi yake Mashariki mwa mji mkuu Damascus na kuwakomboa wanajeshi wapatao 200, huku vikosi vitiifu kwa rais Bashar al Assad vikizidi kusonga mbele dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Uturuki na washirika wake.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jeshi la Syria limevunja mzingiro uliokuwa umewekwa na waasi kuizunguka kambi yake Mashariki mwa mji mkuu Damascus na kuwakomboa wanajeshi wapatao 200, huku vikosi vitiifu kwa rais Bashar al Assad vikizidi kusonga mbele dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Uturuki na washirika wake.

Jeshi la Syria limevunja kabisa mzingiro uliokuwa umewekwa na waasi kuizunguka kambi yake Mashariki mwa mji mkuu Damascus, na kuwakomboa wanajeshi wapatao 200. Wakati huo huo vikosi vitiifu kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad vinasonga mbele kuingia katika ngome za mwisho za waasi katika mkoa wa Idlib unaopakana na Uturuki. 

Wanajeshi wa kikosi maalumu cha jeshi la serikali wameingia katika kambi hiyo iliyo kwenye kwenye eneo la Ghouta Mashariki, wakisaidiwa na ndege za kivita za Urusi na viongozi wa vita kutoka Iran. Waasi wa kundi la kigaidi la la Ahrar al-Sham waliizingira kambi hiyo mwezi Novemba mwaka jana katika juhudi za kupunguza shinikizo la serikali dhidi ya miji na vijiji vya Ghouta Mashariki vilivyokuwa chini ya udhibiti. Kukombolewa kwa mji huo kumetangazwa na kituo cha televisheni cha al-Ikhbariya kinachomilikiwa na serikali ya mjini Damascus, pamoja na shirika linalofuatilia vita vya Syria.

Kuvunjwa kwa mzingiro huo ni mojawapo ya mfululizo wa mafanikio vinayoyapata vikosi vitiifu kwa serikali ya Syria mnamo wiki za hivi karibuni. Hapo jana vikosi hivyo viliukamata pia mji wa Sinjar, ambao ni kiunganishi muhimu cha miji miwili mikubwa zaidi nchini Syria, Damascus na Aleppo.

Mashambulizi ya serikali katika mkoa wa Idlib ambao una ngome za makundi ya waasi yenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida yalitarajiwa baada ya kushindwa kwa kundi linalojiita Dola la Kiislamu- IS mwishoni mwa mwaka uliopita. Wiki jana, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh imemalizika, na hiyo iliashiria kuwa sasa ni zamu ya  magaidi wenye uhusiano na al-Qaida.

Haijulikana mashambulizi ya sasa mkoani Idlib yanaazimia kufikia malengo gani, lakini inafahamika kuwa kujaribu kuukomboa mkoa mzima kwaweza kuchukua muda mrefu na kusababisha hasara kubwa kwa magaidi na wadhamini wao. Duru za waasi zinakadiria kuwa inachokilenga serikali kwa sasa ni kuikamata kambi ya magaidi ya Abu Zuhour iliyo kwenye ncha ya kusini ya mkoa wa Idlib, na kuisalimisha njia muhimu inayounganisha miji ya Damascus na Aleppo.

Uturuki ambayo inawaunga mkono magaidi, imepeleka waangalizi wa kijeshi katika mkoa wa Idlib, ikiwa sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa kati yake, Iran na Urusi kwa madhumuni ya kupunguza mivutano.

Mwanaharakati mmoja wa upinzani ambaye hakupenda jina lake litajwe, amesema waasi wanajikuta katika wakati mgumu, wakikabiliwa upande mmoja na vikosi vya serikali, na upande mwingine mbinyo wa masalia ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh au Dola ya kiislamu.

Mwisho wa habari / 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky