Majibu ya Iran kufuatia kauli ya mshauri wa wizara ya mambo ya nje ya Emirate

Majibu ya Iran kufuatia kauli ya mshauri wa wizara ya mambo ya nje ya Emirate

Bahram Qasimiy amebainisha kuwa hatua ya kwanza ya kukuza ushirikiano na fungamano, ni kuacha tabia za kutuhumu na kuyazushia mataifa mengine na kuzungumza mambo yasiofidisha jamii na uma, huku wakifumbia macho ukweli uliowazi kuhusu nafasi na athari ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ukanda wa mashariki ya kati

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Iran akinga mazungumzo ya mshauri wa waziri wa mambo ya nje wa Emirate, ambapo alidai kuwa serikali ya Iran inaingilia mambo ya nchi za kiarabu, ambapo msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Ira
n amesema kuwa madai hayo si yakweli na hayana mashiko, huku akiwausia viongozi wa Emirate kutumia akili na heshima wanapo amiliana na mataifa mengine, na kuacha kudai madai yasiokuwa na mashiko na tija njema, nakuwataka kuzungumza ukweli na uhakika katika mazungomzo yao.
“Bahram Qasimy” amebainisha na kusema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaungwa mkono na nguvu za wananchi wake katika kulinda maslahi yake huku ikifanya juhudi ya kulinda umoja, suluhu na amani katika ukanda wa mashariki ya kati kadhalika kukabiliana na siasa za uadui dhidi ya haki ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Aidha amemalizia kwa kusema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesimamia kufanya mazungu chini ya kivuli cha kuheshimiana na kuchunga ujirani mwema katika ukanda wa mashariki ya kati, huku ikiwa na shauku kubwa ya kuweka uhusiano salama unaoendana na misngi ya kiakili na majirani wote, na ameyataka mataifa mengine kuyafahamu mazingira yaliopo sasa duniani.
Amesema hatua muhimu ya awali ya kutaka kukuza fungamano zuri, ni kuacha tabia ya kutuhumu mataifa mengine na kufanya mambo yasiokuwa na tija njema katika kupinga mambo yaliokuwa wazi ya athari ya Iran katika kuleta usalama na amani katika mataifa ya mashariki ya kati.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky