Makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wakimbia mji wa Musol na Raqqa

Makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wakimbia mji wa Musol na Raqqa

Idadi kubwa ya makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wameonekana kukimbia miji ya Musol na Raqqa na kuelekea mji wa Mayadin nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo vya habari vya Syria vimeripoti kutoroka kwa idadi kubwa ya makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika miji ya Musol na Raqqa.
Hali hiyo imetokea baada ya ushindi wa mara kwa mara wanaoupata wanajeshi wa Syria na Iraq katika mji wa Musol, ambapo kikundi cha kigaidi cha Daesh mpaka sasa kimeshindwa katika sehemu hiyo, ambapo kwa upande mwingine mashambulio makali ya majeshi ya umoja wa kukabiliana na ugaidi nchini Syria katika mji wa Raqqa iiopo katika mkoa wa Deir ez-Zor nchini humo, ambapo mkoa wa Deir ez-Zor upo upande wa mashariki mwa Syria katika mipaka ya nchi hiyo na Iraq.
Majeshi ya Marekani na nchi kadhaa zinazounda umoja wao wakukukabiliana na ugaidi, waliingia nchini humo mwaka 2014 kwa madai ya kwamba wanataka kukabiliana na kikundi cha Daesh bila yakufuata mpango wa Umoja wa Mataifa, pia bila yakutaka ushirikiano na serikali ya Syria.
Aidha umoja mpaka sasa umesababisha kuuwawa kwa wananchi wengi wa nchi hiyo wasiokuwa na hatia katika mkoa wa Raqqa, Deir ez-Zor na Aleppo na kuharibu miundombinu ya miji hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky