Makombora ya Hizbullah yanaweza kuharibu uchumi wa Israel

Makombora ya Hizbullah yanaweza kuharibu uchumi wa Israel

Mwanajeshi mmoja wa ngazi zajuu katika majeshi ya utawala haramu wa Israel amethibitisha kuwa maeneo ya uchumi wa Israel unaweza kuharibiwa na makomboara ya majeshi ya Hizbullah muda wowote

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: tovuti ya “Walla” ambayo iko chini ya utawala haramu wa Israel, ikinukuu kutoka kwa mwanajeshi mmoja wa ngazi za juu katika jeshi la bahari la Israel , eneo la bahari ambalo linatumiwa na Israel katika masuala ya uchumi zinaweza zikaharibiwa na makombora ya majeshi ya Hizbullah.
Tovuti hiyo imeeleza kuwa: Hizbullah inaweza ikatumia makombora hayo kuripua viwanda vya kuzalisha Gesi vya utawala haramu wa Israel nakuingiza hasara kubvwa kwa utawala huo, kadhalika makombora hayo yanaweza kusimamisha sekta muhimu ya uchumi wa Israel.
Mwanajeshi huyo wa ngazi zajuu katika utawala wa Israel amesema: hofu yetu kuwa ni ongezeko la nguvu za majeshi ya Hizbullah nchini Lebanon nakuwendelea kwa misaada ya kijeshi kutoka Iran kwa kikundi hicho ikiwemo vifaa vya kijeshi ambavyo vinaweza kuisambaratisha Israel.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky