Makumi ya wananchi wauliwa kinyama na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria

Makumi ya wananchi wauliwa kinyama na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria

Kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria kumeuwa makumi ya wananchi wa Syria baada ya kushambulia kijiji cha “Akaribu Safia” kiliopo mashariki mwa mkoa wa Hama nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jinai za kikundi cha kigaidi cha Daesh zazidi kuendelea nchini Syria baada ya kikundi hicho kufanya mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia katika vijiji vya nchi hiyo.
Aidha kikundi cha kigaidi cha Daesh kimefanya mashambulizi ya kinyama katika sehemi ya kijiji “Akaribu Safia” kiliopo sehemu ya Homeh ya mashariki mwa mkoa wa Hama nchini Syria.
Magadi wa kikundi cha Daesh baada ya kuingia katika kijiji hicho waliwakamata wananchi wa kijiji hicho ambao si katika wanajeshi, ambapo asilimia kubwa ni wanawake na watoto, hatimaye kuwauwa wote kwa pamoja bila ya huruma.
Kufuatia shambulio hilo la kikatili inasadikiwa kuuwawa watu 20 na wengine 40 kujeruhiwa na mpaka sasa wako katika hali mbaya, huku habari zikiashiria kuwa miili ya watu waliouwawa na kujeruhiwa imepelekwa katika hospitali ya Salmiyah na Hama nchini humo. Baada ya kuwauwawa tu hao na kukiteka kijiji hicho walipola mali za wananchi wa kijiji hicho.
Kijiji cha Akaribu Safia kipo pembezoni mwa mji wa Salmiyah mashariki mwa mkoa wa Hama, ambapo mkoa wa Hama uko chini ya majeshi ya Syria, huku kikundi cha kigaidi cha Daesh kipo katika maeneo ya Homeh ya mashariki ya mkoa huo, na baadhi ya mida hushambulia maeneo ya makazi ya watu sehemu hiyo.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky