Mamia ya magaidi wa Daesh wajisalimisha kwa Wakurdi nchini Iraq

Mamia ya magaidi wa Daesh wajisalimisha kwa Wakurdi nchini Iraq

Mmoja kati ya viongozi wa vyombo vya usalama sehemu wanayoishi Wakurdi nchini Iraq ametoa taarifa ya kujisalimisha kwa magaidi wa Daesh kwa majeshi yao wiki iliopita

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: kiongozi wa masuala ya ulinzi na Usalama katika maeneo yanayokaliwa na Wakurdi nchini Iraq amesambaza habari yakuwa mamia ya magaidi wa Daesh wamejisalimisha kwa majeshi yao wiki iliopita nchini humo.
Aidha amesema: baada ya ushindi waliofikia majeshi ya serikali ya Iraq dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Hawij, idadi kubwa ya magaidi wa kikundi cha Daesh wamekwenda katika maeneo yanayokaliwa na Wakurdi nchini Iraq na kujisalimisha kwa majeshi yao.
Kiongozi huyo wa vyombo vya usalama katika sehemu za Wakurdi nchini Iraq amebainisha kuwa: kwa uchache magaidi zaidi ya elfu moja wiki iliopita wamejisalimisha, ama inavyoonyesha ni kwamba wote si magaidi, huku akisisitiza baada ya uchunguzi kufanyika kila kitu kitafafanuliwa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky