Mamia ya wakazi wa Raqqah wawarejea katika makazi yao

Mamia ya wakazi wa Raqqah wawarejea katika makazi yao

Mamima ya wakimbizi wa mji wa Raqqah nchini Syria warejea katika makazi yao katika moja ya miji ya sehemu hiyo baada ya kukombolewa na kuteguliwa mabomu yalikuwa yametegewa na vikundi vya Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya serikali ya Syria wametangaz kuwa: mamia ya wakazi waliokuwa wamekimbia makazi yao katika mji wa Raqqa sasa wameanza kurejea katika maeneo yao yaliopo katika mji wa Raqqah baada ya vikundi vya kigaidi vya Daesh kusambaratishwa katika sehemu hiyo.
Kiongozi wa habari na uenezaji katika majeshi ya Syria amesema kuwa baada ya kuukomboa mji wa Raqqah kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, tumeanza hatua ya pili ya kuandaa mazingira ya kurejea kwa wakimbizi waliokuwa wamekimbia makazi yao katika maeneo ya Raqqah, ili familia hizo ziweze kurejea katika makazi yao kwa haraka zaidi, ambapo mamia ya wakazi wa baadhi ya sehemu hiyo wamerejeshwa katika makazi yao ikiwa ni awamu ya kwanza ya mpango huo.
Inasemekana kwamba majeshi ya serikali ya Syria kuwa harakati za kusavisha maeneo yaliokombolewa zimekuwa nzito kutokana na vikundi vya kigaidi vya Daeshi kutega mabomu katika maeneo hayo jambo linawafanya wachelewe kuwarejesha wakazi wake mpaka watakapo maliza kazi ya kutegua mabomu katika maeneo hayo, huku akisisitiza kuwa maeneo yaliokwesha teguliwa ndio hayo ambayo wamerejeshwa wakazi wake.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky