Mapigano kati ya wanajeshi na magaidi yaendelea kusini mwa Ufilipino

Mapigano kati ya wanajeshi na magaidi  yaendelea kusini mwa Ufilipino

serikali ya Ufilipino leo imeadhimisha siku ya uhuru kwa kupandisha bendera ya taifa katika mji wa kusini wa Marawi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali ya Ufilipino leo imeadhimisha siku ya uhuru kwa kupandisha bendera ya taifa katika mji wa kusini wa Marawi, ambako wanajeshi wanaendelea na mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kigaidi wanaoushikilia mji huo. Wakati wa sherehe hiyo milio ya milipuko ilikuwa kisikika kutoka mbali na mahala pa tukio. Maafisa wa kijeshi wanasema jumla ya wanajeshi na polisi 58, magaidi 191 na raia 21 wameuwawa katika mapigano hayo ya wiki tatu sasa. Wakati huo huo Rais Rodrigo Duterte aliwaambia waandishi habari jana kwamba aliamua kutangaza sheria ya kijeshi katika theluthi moja ya eneo la kusini mwa nchi hiyo ili kuwazuia watu wenye silaha kutoroka kutoka Marawi au kufanya mashambulizi mapya maeneo mengine.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky