Mapigano yaendelea Ghouta Mashariki licha ya makubaliano ya kusimamisha vita

Mapigano yaendelea Ghouta Mashariki licha ya makubaliano ya kusimamisha vita

Tangazo la Urusi la kusitisha mashambulizi Syria liloanza Jumanne ili kuingizwe misaada ya kiutu limeshindwa kuzuia vurugu Ghouta Mashariki. Huku Kukishuhudiwa mashambulizi makali ya anga baada ya waasi kurusha makombora mengi katika mji mkuu wa Syria, Damaskas.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Tangazo la Urusi la kusitisha mashambulizi Syria liloanza Jumanne ili kuingizwe misaada ya kiutu limeshindwa kuzuia vurugu Ghouta Mashariki. Huku Kukishuhudiwa mashambulizi makali ya anga baada ya waasi kurusha makombora mengi katika mji mkuu wa Syria, Damaskas.

Siku tisa baada ya vikosi vya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi kuongeza mashambulizi dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na nchi za magharibi, makubaliano ya kusitisha mapigano yaliwapa matumaini raia ambao walikuwa wakijificha kwenye vyumba vya chini vya nyumba zao lakini waasi walivunja makubaliano hayo kwa kurusha makombora upande wa serikali.

Lakini siku ya kwanza ya usitishwaji mapigano wa masaa matano ulioamrishwa Jumatatu na Rais Vladimir Purtin wa Urusi na kuanza saa tatu asubuhi iligubikwa na vurugu nzito.

Serikali ya Syria kwa upande wake imejitetea kwa kusema inachokifanya Ghouta Mashariki ni kuwakomboa wananchi kutoka katika ukatili wa makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za magharibi.

"Haya ni makundi ya kigaidi, hawajali watu, hawajali watoto, wanajaribu kupotosha maoni ya umma wa kimataifa. Tunachojaribu kufanya ni kuwakomboa watu wa Ghouta  Mashariki kutokana na makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa huko kwa miaka sita hadi saba iliyopita," amesema Faisal Mikdad, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria.

Mashambulizi bado yanaendelea siku ya pili ya kutangazwa kusitishwa

Na siku ya Jumatano vikosi vya serikali ya Syria vimeripotiwa kudhibiti maeneo kadhaa mashariki mwa Ghouta vikishirikiana na makundi ya wanamgambo katika mapigano dhidi ya waasi, licha ya mpango wa Urusi wa kusitisha mapigano.

Jumanne ambayo ilikuwa siku ya mwanzo ya makubaliano hayo, Urusi ilionekana kushindwa kutimiza lengo lake la kusitisha mapigano ikiwa ni mpango unaotegemewa kuendelea kwa siku 30 zijazo, kufuatia makubaliano yaliyofikiwa katika Braza la Usalama la Umoja wa Mtaifa. Wakazi 400,000 wa eneo hilo pia wameonekana kukosa imani na mpango huo.

Tangazo hilo la kusitishwa mapigano kwa masaa matano halikuleta amani yoyote Mashariki mwa Ghouta.

Mashambulizi ya mabomu yalifanyika katika eneo la Jisreene ambapo magaidi walikuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya seriklai. Usitishwaji mapigano uliosimamiwa na Urusi ulianza saa tatu asubuhi na kumalizika saa nane mchana.

"Usitishwaji mashambulizi ulikuwa ni wakuchekesha. Waliambiwa ni usitishwaji mapigano wa kuruhusu kuingizwa misaada ya kiutu lakini waliwaruhusu washirika wao kurusha mabomu na kufanya mashambulizi ya anga," amesema Daktari Mohammed kutoka Ghouta Mashariki.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Jumatano mchana kujadili hali ya kibinadamu nchini Syria na litazungumza na kumsikiliza mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock.

Mwisho wa habari / 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky